Page 45 - Fasihi_Kisw_F5
P. 45
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
MDADISI
Ni mafunzo yapi hayo, ya hekima na ubora?
Yatiayo wangu moyo, kwa jitihada na ghera,
FOR ONLINE READING ONLY
Ufanisi yaletayo, ya kugeuza majira,
Maana yake ngonjera, nambie nami nijue.
JAWABU
Mafunzo yatolewayo, kwa usemi wa hadhara,
Mema yachangamshayo, kwa tabasamu ya sura,
Ni ghibu itumikayo, kwa fikira na busara,
Maana yake ngonjera, ni mafunzo kwa shairi.
Ngonjera za Ukuta: Kitabu cha Kwanza (Mnyampala, 1970:5)
(iii) Ushairi wa kidrama
Huu ni ushairi unaotumiwa katika baadhi ya tamthiliya kama mtindo mmojawapo
wa kuandika mazungumzo ya wahusika. Hivyo, hauwezi kutenganishwa na fani
ya tamthiliya (Mulokozi, 2017). Ufuatao ni mfano wa ushairi huu:
Mwanamke
Ndugu zangu, pulikeni ndugu zangu
Sasa si kama zamani
Sasa umetawala uwazi
Uwazi na utambuzi
Tusipigwe na bumbuwazi
Tusijisabilie kirahisi
Kwa ndoa yenye wasiwasi!
Mume mwenyewe kumwakisi
Bali hukufanya kisisi
Ukanipa mchumba mwenye ukakasi…
34 Kitabu cha Mwanafunzi
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 34 23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 34