Page 41 - Fasihi_Kisw_F5
P. 41
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
Vipera vya ushairi andishi
Ushairi andishi umegawanyika katika vipera vitatu. Vipera hivyo ni mashairi,
tenzi na ushairi wa maigizo.
(a) Mashairi
FOR ONLINE READING ONLY
Kuna mitazamo miwili inayohusu mashairi: mtazamo wa kimapokeo na mtazamo
wa kisasa.
Mtazamo wa kimapokeo
Huu ndio mtazamo wa awali kuhusu mashairi ya Kiswahili. Wafuasi wa mtazamo
huu wanasisitiza mambo yafuatayo: kanuni za urari wa vina na mizani, na lugha
nzito ya mkato. Urari wa vina na mizani hulifanya shairi liimbike kwa urahisi
kwa mahadhi yanayofahamika. Tazama mfano wa beti zifuatazo:
Maisha
Maisha kitendawili, kitegue kwa busara,
Uitulize akili, huku ukiwa tohara,
Uhimili kila hali, yaweza kwako kung’ara,
Tukiimudu subira, maisha hayatuwengi.
Maisha kama bahari, yenda mpera mpera,
Vyovyote uwe tayari, kwa kujiweka imara,
Na kumuomba Kahari, akunyooshee dira,
Tukiimudu subira, maisha hayatuwengi.
Maisha ni kujituma, ili uipate tira,
Ushughulike kulima, au kuunda minara,
Mwiko kujiweka nyuma, utakumbwa na idhara,
Tukiimudu subira, maisha hayatuwengi.
Diwani ya Tunzo ya Ushairi ya Ebrahim Hussein (Juma (Mwana
wa Nyasa), 2016).
30 Kitabu cha Mwanafunzi
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 30
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 30 23/06/2024 17:54