Page 38 - Fasihi_Kisw_F5
P. 38
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
Baadhi ya sifa za maigizo ya watoto ni kuwa na muundo wa moja kwa moja na
kutohitaji maleba mahususi.
Shughuli ya 2.7
Tumia vyanzo mbalimbali kuchunguza michezo mitatu ya watoto, kisha bainisha
FOR ONLINE READING ONLY
mbinu za kisanaa zilizotumika katika utunzi wa michezo hiyo.
Zoezi la 2.1
1. Kwa kutumia mifano fasili dhana zifuatazo:
(a) hurafa (b) soga (c) lakabu
(d) istiara (e) visasuli (f) hekaya
(g) ngomezi
2. Kwa kutumia mifano, eleza tofauti kati ya ngano na vigano.
3. Kwa kutumia mifano anuwai, tofautisha vichekesho na maigizo.
4. Jadili athari za utani unaofanyika katika jamii yako.
5. “Si kila mchezo wa watoto ni fasihi simulizi.” Jadili kauli hii kwa hoja
maridhawa.
6. Kwa kutumia mifano, tofautisha dhana zifuatazo:
(a) tendi na tenzi
(b) maghani na nyimbo
(c) visasili na visakale
(d) vitendawili na mizungu
(e) visasili na visasuli
7. Chambua mbinu za kisanaa zinazojitokeza katika ngano, visasili, na
soga.
8. Sikiliza ngano mbili kutoka kwa wenzako kisha andika insha fupi
kueleza mafunzo yaliyomo katika ngano hizo.
Kitabu cha Mwanafunzi 27
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 27 23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 27