Page 37 - Fasihi_Kisw_F5
P. 37
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
Ta la la la la la
Kiota
Wimbo wa mchezo huu huambatana na vitendo vya kutembea na kuzunguka.
FOR ONLINE READING ONLY
Michezo mingi ya watoto hujumuisha pamoja nyimbo na vitendo.
Maigizo ya watoto ni aina nyingine ya michezo ya watoto. Watoto huigiza michezo
inayoakisi mazingira yanayowazunguka kama vile nyumbani, shuleni, shambani,
hospitalini, barabarani, kanisani, msikitini na porini. Pia, watoto huigiza mambo
wanayoyaona kwenye runinga, hasa watoto waishio mijini. Kwa mfano, huigiza
michezo ya kivita, sherehe mbalimbali, vikundi vya nyimbo, miziki na michezo
ya kuigiza.
Maigizo ya watoto, kama ilivyo kwa kazi nyingine za fasihi, yana vipengele
vya fani na maudhui. Maudhui ya michezo ya watoto, kwanza, huhusu maisha
ya nyumbani kwa sababu ndiyo maisha wanayoyaona mara kwa mara. Watoto
huigiza maisha ya nyumbani kwa kuakisi maisha halisi ya familia, hususani
yale wanayoyaona kwenye kaya zao. Mathalani, kama baba au mama ni mkali,
mtoto atakayewaigiza, ni lazima atakuwa mkali, pengine kuzidi ukali anaouona
kwa wazazi wake; vivyo hivyo, kama baba au mama ni mpole na mkarimu basi
muigizaji ataigiza upole na ukarimu wao. Ikiwa mzazi ni mchapakazi, basi
muigizaji atakuwa na tabia hiyo. Kama ni nadhifu, mwigizaji naye atajitahidi
kuwa nadhifu. Kwa hiyo watoto waigizao nafasi ya wazazi wao, huakisi tabia ya
wazazi hao.
Kwa kawaida, hakuna matini inayokuwa imeandaliwa kabla ya mchezo, bali
maigizo ya watoto hubuniwa papo kwa papo. Watoto wanapokutana hukubaliana
aina ya mchezo na kugawana majukumu ya kila mhusika; wakati mwingine,
watoto wenyewe huchagua nafasi watakazoigiza. Uigizaji wa michezo ya watoto
huambatana na ubunifu ambapo kila mtoto (mhusika) hubuni uigizaji wa uhusika
wake. Katika maigizo yanayohusisha wanyama, kwa mfano, kama igizo lina
mhusika simba, mtoto anayeigiza kama simba ni lazima awe na sifa za ubabe,
sauti nzito na nguvu. Halikadhalika, atakayeigiza kama jogoo, awe na sauti kali
ili atakapowika asikike.
Aidha, watoto huchagua nafasi kulingana na uwezo wao na jinsi jamii ilivyoainisha
majukumu mbalimbali kama ya udaktari, ualimu, uaskari na mengineyo. Kwa
hiyo, watoto huchagua nafasi za kuigiza kutokana na kazi wazipendazo. Wakati
mwingine kupitia michezo hii, ndoto za watoto huchomoza na watoto wengine
huanza kuishi na ndoto zao.
26 Kitabu cha Mwanafunzi
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 26 23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 26