Page 35 - Fasihi_Kisw_F5
P. 35
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
Kama ilivyodokezwa katika maelezo ya sanaa za maonesho kwa ujumla,
vichekesho ni mojawapo ya sanaa mamboleo; vichekesho vingi vimetokana
na kuletwa kwa tamthiliya za kizungu zilizobeba na kuongelea utamaduni wa
kimagharibi. Baadhi ziliongelea matatizo ya kijamii ya wakati wa ukoloni,
FOR ONLINE READING ONLY
mathalani suala la mgongano kati ya miji na vijiji, na uzuzu au ushamba wa
Mwafrika anayetoka kijijini na kuingia mjini kwa mara ya kwanza. Maigizo hayo
hayakuwa na maana kubwa kwa Waafrika zaidi ya kuwachekesha kupitia katika
vitendo vilivyofanywa kwenye jukwaa. Kwa hiyo, Waafrika wakadhani kuwa
jambo muhimu katika vichekesho ni kuchekesha.
Kimsingi, dhima ya vichekesho si kuchekesha tu, bali vichekesho huelimisha pia.
Mifano ya vichekesho ni kama ile inayopatikana katika vipindi vinavyorushwa na
vituo vya redio, mitandao ya kijamii, na runinga. Mifano ya vipindi vya kwenye
runinga ni Mizengwe (ITV), Futuhi (Star TV), Vitimbi Show (Channel Ten), na
Kitimtim (DSTV).
(d) Ngomezi
Hii ni sanaa ya kuwasiliana kupitia midundo ya ngoma. Baadhi ya jamii hupeana
taarifa za matukio mbalimbali kupitia ngoma. Aghalabu, taarifa hizo huwa katika
hali ya mafumbo, kiasi kwamba, wenyeji wa jamii husika tu huweza kubaini
maana ya midundo husika. Hii yatokana na ukweli kuwa midundo katika sanaa
hii hufuata kanuni maalumu zinazojulikana na wanajamii hao tu. Kanuni hizo
hubebwa kupitia vipengele vya aina ya ngoma zinazotumika, muda wa kupigwa
kwa ngoma pamoja na kasi au mwachano wa upigaji. Kanuni hizi huwasaidia
wanajamii kupata ujumbe unaowasilishwa. Kwa mfano, katika jamii ya Wayao
kuna ngoma inayojulikana kama Ngula-ntwe inayopigwa kwa ajili ya kutoa
ujumbe kuhusu matukio mbalimbali ya kitanzia. Kutokana na mapigo na
midundo ya ngoma, ujumbe huo huweza kufasiliwa kuwa: “Simba amevamia
na kuua mifugo”, “Simba amejeruhi mtu ila hajamuua”, “Simba ameua mtu”, au
“Kesho wanaume wote wanatakiwa kwenda kwenye msako wa simba mvamizi.”
(e) Utani
Ni hali ya kufanyiana mizaha au masihara baina ya watu ambapo hali hii ni tofauti
na desturi za kutokuheshimiana. Wanajamii wenye uhusiano wa kutaniana,
hutaniana mahali popote wakutanapo kama vile msibani, harusini, hata kwenye
sehemu za kazi. Utani huweza kuwa kati ya mtu na mtu, ukoo na ukoo au kabila
na kabila. Utani kati ya mtu na mtu huwa kati ya babu/bibi na wajukuu, mtu
na shemeji au wifi na wifi. Kadhalika, utani kati ya kabila na kabila, aghalabu,
huwa kati ya makabila yenye asili ya kuishi katika eneo moja au yaliyokuwa na
24 Kitabu cha Mwanafunzi
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 24 23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 24