Page 30 - Fasihi_Kisw_F5
P. 30
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
Shida yako ni rupia, takujalia fulusi
Hebu njoo Jumamosi, bado nashauri moyo
Mkopaji
FOR ONLINE READING ONLY
Hodi Bwana nawasili, kwa ile yetu miadi
Unihesabie mali, arubani nakidi
Muaminishe Jalali, nifanyie itikadi
Tafadhali nikopeshe, haondoe shida yangu
Mkopwaji
Moyo wangu siamini, kukuhesabia mali
Shuruti lete dhamini, ambaye msema kweli
Shilingi arubaini, kulipa huna dalili
Hebu njoo Jumapili, bado nashauri moyo
Ngonjera za Ukuta: Kitabu cha kwanza (Mnyampala, 1967:22)
(c) Tenzi
Tenzi ni tungo ndefu zinazoeleza tukio fulani linalotokea au lililowahi kutokea
katika jamii; au zinazofafanua jambo au fikra fulani. Tenzi huwa na kisa kimoja
kinachoelezwa kwa kina. Kisa hicho kinaweza kuwa maelezo kuhusu wasifu
wa mtu fulani, jambo fulani la kihistoria au jambo lolote. Sifa ya kusimulia au
kuelezea jambo kwa urefu ndio husababisha tenzi kuwa na beti nyingi kuliko
mashairi au aina nyingine za ushairi.
Utendi ni utungo wenye masimulizi marefu kuhusu matendo ama matukio
ya kishujaa na wasifu wa mashujaa. Utenzi na tendi huwa na muundo wenye
kufungamana na mahadhi ya ala ya muziki inayotumika au melodia ya uimbaji.
Kwa kawaida, hazina urari wa vina na mizani. Tenzi zenye urari wa vina na mizani
ni zile zenye kufuata kanuni za ushairi andishi wa Kiswahili japo chimbuko au
utungaji wake ni wa kisimulizi. Mifano ya tenzi hizo ni Utenzi wa Nyakiiru Kibi
(Mulokozi, 1997) na Utenzi wa Mwanakupona. Mfano wa tendi ni Utendi wa
Fumo Liyongo (Kijumwa, 1913) katika Tenzi Tatu za Kale (Mh. Mulokozi, 1999).
Katika tenzi hizo, mishororo haikugawanywa katika vipande viwili. Kila ubeti
huwa una mistari minne; mistari mitatu ya kwanza ikiwa na vina vyenye urari na
ule wa mwisho ukiwa na kina tofauti. Pamoja na vina hivyo kuwa na urari sawa,
hubadilika toka ubeti mmoja hadi ubeti mwingine. Kina kinachorudiwa katika
Kitabu cha Mwanafunzi 19
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 19 23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 19