Page 26 - Fasihi_Kisw_F5
P. 26
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
(c) Mizungu
Mizungu ni kauli zenye mafumbo zinazoonesha ukinzani wa fikra au tukio.
Mbali na vitendawili vya kawaida, kuna vitendawili vingine vijulikanavyo kama
mizungu. Mizungu hii hutumia zaidi mafumbo. Kwa mfano, inaelezwa kwamba
FOR ONLINE READING ONLY
mtu hawezi kumwoa ndugu wa damu. Ukinzani huu umetumika kuonya ndugu
wasiwe na uhusiano wa kimapenzi. Mizungu hutumia mafumbo ya hali ya juu,
kwa hivyo hutumiwa na watu wazima katika miviga ili kueleza dhana na mawazo
mbalimbali kwa maongezi au nyimbo. Mifano mizuri ya mizungu inayohusu
jambo hili ni:
(i) Ua zuri sana limeota kwenye miiba; hivyo, huwezi kulichuma.
(ii) Papai limeiva nyumbani, ila siwezi kulila.
Mizungu hutumia lugha ya picha inayoonesha ukinzani wa fikra. Ukinzani
husaidia kumfikirisha msikilizaji na kumpa changamoto ya kutafuta jibu. Mifano
mizuri ya mizungu ni:
(i) Adui rafiki (moto)
(ii) Nimezishika lakini siwezi kuzitumia (mhasibu na fedha)
(d) Mafumbo
Mafumbo ni kauli au maelezo yanayoficha maana ambayo humtaka msikilizaji
kuyafumbua. Kwa mfano, watu wanamteta mtu, ikitokea mtetwaji anakuja mahali
hapo, mmoja wao anaweza kusema wifi kaja au shangazi kaja. Hii huwasaidia
kubadilisha maongezi baada ya kufumbua wifi au shangazi kuwa ndiye mtu
anayetetwa ingawa mtu huyo si wifi wala shangazi wa mtu yeyote katika kundi
hilo.
Aidha, kwenye mazingira ambapo watu wanaongea lakini hawataki mmoja
wao ajue maongezi yao, labda kwa sababu ni domokaya, mmoja wao anaweza
kuwatahadharisha wenziwe kwa kusema hivi, Ooho! Mkorosho umeanguka!
Inabidi waelewe kwamba “mkorosho ulioanguka” ni mmoja wao. Hivyo,
wataongea kwa tahadhari kubwa. Aghalabu, mafumbo mengi huwa ni kejeli dhidi
ya watu wenye tabia mbaya. Mafumbo yana malengo ya kuelimisha, kuwezesha
mawasiliano, kuburudisha, kukosoa na kuonya kuhusu mambo yanayotendeka
miongoni mwa wanajamii.
(e) Vitendawili
Vitendawili ni semi fupifupi za mafumbo zenye kutumia lugha ya picha, tamathali
na ishara kueleza jambo lililofichika. Jambo hilo ndilo jibu la fumbo. Kwa
Kitabu cha Mwanafunzi 15
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 15 23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 15