Page 24 - Fasihi_Kisw_F5
P. 24
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
Kwa mfano, kigano kinaweza kueleza kuhusu mzazi aliyempenda mno mtoto
wake wa pekee kiasi cha kutothubutu kumkemea au kumrudi. Hatimaye, mtoto
alijenga tabia mbaya. Basi, msimulizi husema kwa methali: Mchelea mwana
kulia hulia mwenyewe.
FOR ONLINE READING ONLY
Aghalabu, vigano hutokea katika mazungumzo na, wakati mwingine, hutungwa
papo hapo. Kwa mantiki hiyo, vigano vingi huwa havienei kwa sababu
hufungamanishwa na muktadha wa maongezi na hutungwa kwa ajili ya mada
husika tu. Kwa hiyo, hupotea baada ya mada kuwasilishwa.
(e) Soga
Soga ni hadithi fupifupi za utani na ucheshi. Hadithi hizi husimuliwa kwa
mfuatano wa matukio yanayochekesha. Soga hujengwa juu ya tukio moja tu.
Tukio hilo, aghalabu, hulenga kuchekesha kwa kubeza na kukejeli. Pia, hueleza
mambo ya ukweli unaoumiza kwa njia ya ucheshi ili kupunguza ukali wa ukweli
huo. Soga hupatikana au hufanywa na watu wa jamii zenye historia ya kufanyiana
utani kama vile jamii za Wanyaturu na Wakurya, Wahaya na Waha, Wachaga na
Wapare. Kwa ujumla, soga hujikita katika kuburudisha na, wakati mwingine,
kuelimisha jamii. Tazama mfano wa soga inayowahusu Wamakonde hapa chini:
Kisa cha Mmakonde na Ngedere
Mmakonde mmoja alikwenda shambani kwake, akamkuta ngedere akila
mahindi shambani mwake. Ngedere alipomwona Mmakonde akakimbilia juu
ya mti. Mmakonde akamwona kule alikojificha, akamwambia: “Wee ngedere
nimechakuona; uchijifanye n’janja, telenka hapa chini nikupige nchale ili
upate adhabu moja tu. Vinginevyo, n’kupige nchale ukiwa hukohuko juu ya
nti, upate adhabu mbili: Adhabu ya kupigwa nchale, na adhabu ya kuanguka
kutoka juu ya nti baada ya kupigwa nchale. Je, wewe ungekuwa ngedere
ungefanyaje?
Shughuli ya 2.3
Tumia vyanzo vya mtandaoni na maktabani, kufafanua semi na vipera vyake kwa
kuzingatia maana na sifa.
Semi
Semi ni tungo fupifupi za fasihi simulizi, na aghalabu, hutumia picha, tamathali
na ishara. Semi hutumika kutoa mafunzo, nazo zimegawanyika katika vipera
mbalimbali kama vile methali, misemo, mizungu, mafumbo, na vitendawili.
Kitabu cha Mwanafunzi 13
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 13 23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 13