Page 19 - Fasihi_Kisw_F5
P. 19
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
(a) Ngano
Ngano ni hadithi za kimapokeo zitumiazo wahusika kama wanyama, miti na
watu. Ni kipera cha mwanzo kabisa katika utanzu wa hadithi. Kwa kawaida,
mtunzi wa ngano hajulikani. Ngano hupokezanwa na kuendelezwa kutoka kizazi
FOR ONLINE READING ONLY
hadi kizazi. Maudhui yake hujikita katika maadili, uhusiano na mwenendo mzuri
katika jamii. Aghalabu, ngano ni hadithi za burudani ambazo husimuliwa katika
mazingira ya starehe na mapumziko. Ngano ina vipera vidogo kadha. Baadhi ya
vipera hivyo ni kisasuli, hurafa, hekaya na istiara.
Kisasuli
Kisasuli ni hadithi ya kisanaa yenye kueleza usuli na sababu za jambo, tukio
au hali. Mathalani, zipo hadithi zinazoeleza kwa nini mnyama fulani anapenda
kushirikiana na wanadamu au ameumbika kwa namna fulani. Tazama mfano wa
kisasuli cha hadithi ya “Kwa nini nyoka hana miguu?”
Kwa nini nyoka hana miguu?
Siku moja Nyoka pamoja na wanyama wengine walialikwa kwenye sherehe
nyumbani kwa mfalme. Kule walikula na kunywa! Baadaye mfalme
aliwaita ili wapewe zawadi. Kwa sababu ya uroho wake, Nyoka hakusikia
wito. Alipozinduka, alikuta miguu yote, hata ile hafifu ya Tandu na Buibui,
imeshatolewa; akabakia anajiburuza kwa tumbo lake. Mpaka leo hii nyoka
hana miguu (Balisidya, 1987).
Hurafa ni ngano zenye wahusika wanyama tu. Wanyama hao huwakilisha tabia
na matendo ya binadamu kwa kurejelea masuala yanayopatikana katika jamii.
Maudhui katika hurafa hueleza kuhusu tabia nzuri au mbaya za binadamu, kama
vile woga, ulafi na tamaa. Katika hurafa, wanyama wanaotumiwa ni kama vile
sungura, fisi na kobe. Sungura huwakilisha ujanja, kutokata tamaa na kutochoka.
Fisi huwakilisha tamaa, ulafi, woga, uzembe na ujinga. Kobe huwakilisha
ukimya, busara na utulivu. Aidha, ni mhusika ambaye hufanya vitu kimyakimya
lakini huibuka mshindi. Ufuatao ni mfano wa hurafa:
Sungura na Fisi
Siku moja Sungura alipokuwa matembezini alikutana na Fisi. Fisi alimwangalia
Sungura na kumuuliza, “Wewe unayekodoa macho hivi unaenda wapi, au kuila
nyama yako?” Sungura akamwangalia Fisi na kumwambia, “Nimeambiwa na
Simba nimsubiri hapa ndipo tuandamane hadi kwake nikamtayarishie ini la
Fisi analolitamani sana.” Fisi akamwangalia Sungura na kumwuliza, “Huyo
Simba yuko wapi?” Sungura akaita kwa sauti ya juu, “Simbaaaaaa!”
8 Kitabu cha Mwanafunzi
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 8
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 8 23/06/2024 17:54