Page 20 - Fasihi_Kisw_F5
P. 20
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
Baada ya kuita kwa sauti hiyo, Sungura alijigeuza kidogo, akapiga mluzi na
kusema kwa sauti nzito, “Naja sasa hivi. Naandama nyayo za Fisi aliyepita
hapa. Natamani kumkamata ili nipate ini lake nikuletee ukanitayarishie kama
tulivyoagana. Mara tu Fisi alipoyasikia hayo, aligeuka na kutimua mbio
FOR ONLINE READING ONLY
kuelekea kichakani. Sungura alibaki alikokuwa na kuangua kicheko.
Hekaya ni ngano zenye visa visivyo vya kawaida vinavyoambatana na masaibu
na pengine hata ujanja wa mhusika mkuu ambaye huweza kuwa mtu au mnyama.
Hekaya hujengwa na visa vingi vinavyotofautiana. Mhusika mkuu katika hekaya
hupitia misukosuko mingi hadi kukaribia kushindwa. Hata hivyo, katika hatua za
mwisho kabisa, mhusika huyu huweza kuibuka mshindi kwa namna isiyotarajiwa.
Lengo la hekaya ni kumtia mtu moyo asikate tamaa anapopitia changamoto za
aina mbalimbali. Kimsingi, kinachohimizwa ni kutumia akili kutatua matatizo ya
maisha. Kwa kumtumia mhusika sungura, kwa mfano, tunahimizwa kuwa wajanja
na kutokujidharau hata kama ni wadogo. Umbile dogo linaweza kuwakilisha pia
uwezo wa kiuchumi kama vile kuwa na mtaji mdogo. Mtu anaweza kutumia
mtaji mdogo kufanya biashara mpaka kufikia kiwango cha kuwa mfanyabiashara
mkubwa. Ufuatao ni mfano wa hekaya:
Mfanyabiashara na Wakeze
Hapo zamani, kulitokea mfanyabiashara mmoja aliyekuwa na mali nyingi
sana. Basi alioa mke, baadaye akaongeza mke wa pili (Bi mdogo). Wakaishi
hivyo. Alitokea kumpenda zaidi Bi. Mdogo na kumnyanyasa Bi. Mkubwa
(mke wa kwanza).
Siku moja, alikuwa na safari ya kwenda kununua bidhaa za duka lake. Basi
akamwambia Bi. Mdogo ataje mahitaji yote ambayo angependa aletewe kama
zawadi. Bi. Mdogo akataja vitu vingi. Naam, kwa kuwa mfanyabiashara yule
alikuwa akimpenda sana, hakusita kumhakikishia kwamba angemletea. Kwa
shingo upande, alimwendea vilevile Bi. Mkubwa na kumwambia ataje zawadi
ya kumletea. Yule Bi. Mkubwa akamwambia mumewe asisumbuke ila amletee
pete na kipande cha akili. Basi, kwa dharau yule bwana akakubali.
Basi tajiri yule akafunga safari akafika huko, akanunua vifaa vyake vyote
alivyovihitaji kwa ajili ya duka lake. Vilevile, akanunua vitu vyote kama vile
nguo ambazo Bi. Mdogo alimtuma, pamoja na pete ya Bi. Mkubwa. Sasa
akakwama wapi apate kipande cha akili. Akazunguka maduka yote, asipate.
Mwishowe, akaona ni upuuzi kuendelea kutafuta kipande hicho.
Kitabu cha Mwanafunzi 9
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 9 23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 9