Page 16 - Fasihi_Kisw_F5
P. 16
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
za uzalishaji na kuanza kuwa shughuli maalumu ya kijamii ambapo ilitendwa
katika matukio mbalimbali, kama vile sherehe na ibada.
Nadharia nyingine inayoelezwa na Mulokozi (2017) ni ya mwigo au uigaji.
Nadharia hii inazingatia ubunifu wa mwanadamu katika kuiga maumbile na
FOR ONLINE READING ONLY
mazingira yaliyomzunguka kwa kusawiri vitu vilivyomo katika hali mbalimbali.
Akigusia dosari kuu ya nadharia hii, Mulokozi anasema kuwa katika kusisitiza
mno uigaji, suala la ubunifu wa kisanaa na kifasihi linasahauliwa.
Shughuli ya 1.6
Jadili ubora na upungufu unaojitokeza katika nadharia za chimbuko la fasihi.
Tamrini
1. Kwa kutumia mifano, fafanua maana ya dhana zifuatazo:
(a) Fasihi
(b) Mtazamo
(c) Nadharia
(d) Chimbuko
2. Dhana ya fasihi huelezwa kwa mitazamo mbalimbali. Jadili mitazamo
hiyo.
3. “Ujifunzaji wa fasihi hauna umuhimu wowote.” Jadili hoja hii.
4. Chunguza fasili za dhana ya fasihi zifuatazo kisha, eleza zinafanana na
kutofautiana katika vipengele vipi?
(a) Fasihi inahusisha ufundi wa matumizi ya lugha katika kuwasilisha
dhana na matukio mbalimbali yanayomhusu binadamu na
mazingira yake (Ponera, 2014).
(b) Fasihi ni sanaa ya lugha yenye ubunifu inayosawiri vipengele vya
maisha, mahusiano, mazingira na hisia za watu katika muktadha
fulani (Mulokozi, 2017).
(c) Fasihi ni sanaa itumiayo lugha ili kufikisha ujumbe uliokusudiwa
na unaoendana na jamii husika (Mlaga, 2017).
Kitabu cha Mwanafunzi 5
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 5 23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 5