Page 12 - Fasihi_Kisw_F5
P. 12
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
Sura
ya Dhana na chimbuko la fasihi
Maisha bila FasihiREADING ONLY
Kwanza
Utangulizi
Fasihi inatuwezesha kufikiri kwa kina na kufahamu tamaduni na masuala
mbalimbali ya kijamii pamoja na kuwasiliana kwa ufasaha. Katika sura hii,
utajifunza juu ya dhana ya fasihi, mitazamo mbalimbali ya dhana hiyo ya
fasihi, na chimbuko la fasihi. Umahiri utakaojenga katika sura hii utakusaidia
kukuza uelewa na kutathmini maarifa hayo.
FOR ONLINE
Shughuli ya 1.1
Kwa kutumia vyanzo vya maktabani, mtandaoni, au vinginevyo, bainisha matini
ambazo unadhani ni fasihi, na eleza kwa nini unadhani hivyo.
Dhana ya fasihi
Wataalamu mbalimbali wameielezea dhana ya fasihi kwa namna tofauti. Kwa
ujumla wanakubaliana kuwa fasihi ni sanaa bunifu ya lugha inayosawiri hali
mbalimbali za maisha. Hali hizi ni pamoja na mahusiano, hisia za watu, mazingira,
migogoro na mengineyo. Sanaa ya fasihi inajidhihirisha katika tanzu kama vile
tamthiliya, riwaya, ushairi, semi na nyinginezo.
Shughuli ya 1.2
Kwa kutumia mifano ya fasihi unayoifahamu, toa maoni yako kuhusu dhana ya
fasihi.
Shughuli ya 1.3
Kwa kutumia vyanzo mbalimbali, fafanua mitazamo kuhusu dhana ya fasihi.
Kitabu cha Mwanafunzi 1
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 1 23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 1