Page 13 - Fasihi_Kisw_F5
P. 13
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
Mitazamo mbalimbali kuhusu dhana ya fasihi
Kuna mitazamo mbalimbali inayojadili dhana ya fasihi. Mtazamo wa kwanza
unajiegemeza kwenye kisawe cha neno fasihi kwa kiingereza, yaani literature.
Mtazamo huu unadai kuwa literature ni jumla ya maandishi yote yaani kila kitu
FOR ONLINE READING ONLY
kilichoandikwa ni fasihi. Mtazamo huu umeelezewa na Wellek na Warren (1986),
Hata hivyo, dhana hii inapingwa na baadhi ya wanazuoni wa fasihi. Kwa mfano,
Mulokozi (2017) anadai kuwa dhana ya literature inatofautiana na dhana ya
fasihi. Katika lugha ya Kiingereza, maana moja wapo ya literature ni maandishi
yoyote, ilhali katika Kiswahili, dhana ya “fasihi” inazingatia fasihi kama sanaa
na aina zote za fasihi.
Mtazamo wa pili unadai kuwa fasihi ni hisi ambazo zinajifafanua kwa njia ya
lugha. Wafuasi wakuu wa mtazamo huu ni Sengo na Kiango (1975). Wataalamu
hawa wanasema kuwa ili mwanafasihi aweze kuandika au kueleza jambo kifasihi
lazima aguswe na hisia fulani. Wataalamu hao wanasema kuwa hisi ni kama
kusikia njaa, baridi, joto, uchovu au kuumwa. Mtazamo huu pia umekosolewa na
baadhi ya wanazuoni. Kwa mfano, Mulokozi (2017) anaeleza kuwa mtazamo huu
unachanganya mambo matatu ambayo ni fasihi yenyewe, mambo yaelezwayo
na fasihi, na mtindo wa kifasihi. Kwa mujibu wa mtazamo huu, fasihi inaweza
kuelezea hisi lakini fasihi yenyewe si hisi. Kwa mfano, fasihi huweza kuelezea
hisi za mapenzi lakini fasihi yenyewe si mapenzi.
Mtazamo wa tatu unaitazama fasihi kama sanaa ya lugha yenye ubunifu bila
kujali kama imeandikwa au la. Mtazamo huu unaafikiwa na Kirumbi (1975),
Mutembei (2006) na Senkoro (2011). Kwa mujibu wa mtazamo huu, hata
nyimbo na masimulizi ya kisanaa ni fasihi, ijapokuwa hayakuandikwa. Kirumbi
anasema kuwa fasihi ni taaluma ya sanaa inayowasilishwa kwa njia ya lugha
katika muundo wa maandishi au matamshi. Senkoro (2011) ana mtazamo sawa
na wa Kirumbi anapoieleza fasihi kuwa ni “sanaa itoayo maudhui yake kwa
kutumia lugha ya maneno ambayo hutamkwa ama huandikwa.”
Mtazamo wa nne unadai kuwa fasihi ni maandiko bora ya kisanaa yenye manufaa
ya kudumu. Akizungumzia mtazamo huu, Summers (1989) anasema kuwa fasihi
ni sanaa inayojumuisha zaidi maneno yaliyoandikwa. Mtazamo huu unaupa uzito
ufundi wa kubuni lakini unafinya mawanda ya fasihi kwa kuhusisha mawazo
yaliyo bora tu ambayo, hata hivyo, ni vigumu kuyaainisha.
Mtazamo wa tano unaeleza kuwa fasihi ni matokeo ya matumizi ya lugha kwa
njia isiyo ya kawaida ili kuleta athari maalumu. Miongoni mwa waasisi wa mtazamo
huu Roman Jakobson. Mtazamo huu huona kuwa fasihi hukiuka taratibu za
2 Kitabu cha Mwanafunzi
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 2 23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 2