Page 14 - Fasihi_Kisw_F5
P. 14
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
kawaida za matumizi ya lugha katika sarufi, maana na sauti ili kumvutia na
kumuathiri msikilizaji au msomaji. Mtazamo huu humfanya msomaji aitafakari
lugha yenyewe badala ya kuutafakari ujumbe unaowasilishwa na lugha hiyo.
Vilevile, fasihi inaonekana kuelemea zaidi upande wa fani na kupuuza maudhui,
FOR ONLINE READING ONLY
maana na muktadha wa kazi za fasihi.
Kutokana na mjadala huu, tunaweza kusema kuwa mitazamo hii yote inahusisha
fasihi, maisha na jamii. Yaani, fasihi ni sanaa inayotumia lugha kuwasilishia hali
mbalimbali zinazomhusu mwanadamu na maisha yake. Tunaposema “lugha”
hatuna maana ya usemaji wa kutumia sauti tu, bali hata mawasiliano ya kutumia
ishara na vitendo.
Shughuli ya 1.4
Kwa kutumia vyanzo mbalimbali, jadili ubora na upungufu wa kila mtazamo
kuhusu dhana ya fasihi.
Zoezi la 1
1. Ni kwa vipi si kila andiko ni fasihi?
2. Eleza ni kwa namna gani fasihi ni sanaa.
3. Jadili umuhimu wa fasihi katika maisha ya mwanadamu.
Nadharia za chimbuko la fasihi
Shughuli ya 1.5
Soma matini mbalimbali zinazopatikana mkondoni na maktabani zinazohusu
nadharia za chimbuko la fasihi, kisha zielezee kwa ufupi.
Dhana ya nadharia
Wataalamu wanaeleza kuwa nadharia ni maelezo au mwongozo uliopangwa ili
kusaidia kueleza, kutatua au kutekeleza jambo fulani. Nadharia za chimbuko la
fasihi ambazo Senkoro (1987) na Mulokozi (2017) wanazitaja ni nadharia za
kidhanifu na kiyakinifu.
Nadharia ya kidhanifu
Msingi wa nadharia hii ni mawazo ya kudhani, yasiyotokana na uhalisi. Waasisi
wa nadharia hii ni wanafalsafa wa Kiyunani, wakiwamo Plato na Sokrate. Wafuasi
wa nadharia hii wanaamini kuwa fasihi na sanaa vimetoka kwa Mungu. Hivyo,
mwanafasihi huipokea sanaa ikiwa tayari imeivishwa na Mungu.
Kitabu cha Mwanafunzi 3
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 3 23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 3