Page 17 - Fasihi_Kisw_F5
P. 17
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
Sura
ya Fasihi simulizi na fasihi
FOR ONLINE READING ONLY
Pili andishi
Utangulizi
Fasihi simulizi na fasihi andishi ni sanaa muhimu ambazo mtu huzitumia kwa
malengo ya kujiburudisha, kuelimisha na hata kuhifadhi utamaduni wa jamii.
Katika sura hii, utajifunza kuhusu tanzu na vipera vya fasihi simulizi na fasihi
andishi na pia utajifunza uhusiano uliopo baina ya fasihi simulizi na fasihi
andishi. Aidha, utajifunza kuhusu mchango wa fasihi simulizi katika maendeleo
ya fasihi andishi na mchango wa fasihi kwa jumla katika maendeleo ya jamii.
Umahiri utakaoujenga katika sura hii utakusaidia kuchambua na kutathmini
vipengele mbalimbali katika maisha.
Nyenzo ya kuwasilisha mawazo katika miktadha mbalimbali
Shughuli ya 2.1
Kwa kutumia vyanzo vya mkondoni na maktabani, chunguza tanzu na vipera vya
fasihi simulizi kisha jibu maswali yafuatayo:
(i) Nini tofauti ya utanzu na kipera?
(ii) Kuna tofauti gani kati ya utani na majigambo?
(iii) Kuna tofauti gani kati ya utanzu wa hadithi na semi?
(iv) Sanaa za maonesho zina sifa zipi?
(v) Nini tofauti ya misemo na misimu?
Tanzu na vipera vya fasihi simulizi
Wataalamu mbalimbali (kwa mfano Mulokozi na Wamitila) wamegawanya
fasihi simulizi katika tanzu na vipera mbalimbali ambavyo vimeoneshwa katika
Kielelezo namba 2.1.
6 Kitabu cha Mwanafunzi
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 6
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 6 23/06/2024 17:54