Page 21 - Fasihi_Kisw_F5
P. 21
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
Basi, katika ghadhabu yake, akawa akimtukana huyo Bi. Mkubwa, jinsi
alivyokuwa mpumbavu. Ikatokea kwamba Bi. Kizee mmoja akamsikia
alivyolalamika na kuapiza. Yule Bi. Kizee akamuuliza kwa nini alikuwa
akilalamika. Yule bwana akamsimulia kisa chote. Bi. Kizee akamwambia
FOR ONLINE READING ONLY
yule bwana kuwa asipate taabu kwani kipande hicho anacho nyumbani.
Wakafuatana kuelekea nyumbani kwa huyo Bi. Kizee. Kufika karibu na kule
nyumbani, Bi. Kizee akamweleza kwamba kipande hicho kiko nyumbani kwa
yule bwana, ila tu akitaka kukipata sharti atakapokaribia nyumbani kwake
ajipake kinyesi, halafu aone jinsi wake zake watakavyompokea.
Basi tajiri akafanya kama alivyoagizwa. Alipokaribia nyumbani kwake,
akajipaka kinyesi mwili mzima, akawa hovyo kabisa kisha akabisha hodi
kwanza nyumbani kwa Bi. Mdogo. Bi. Mdogo kufungua mlango katika
harakati za kumlaki, akaona mumewe kajaa kinyesi mwili wote. Bi. Mdogo
akafoka sana na kumwambia asithubutu kuingia mle ndani hadi awe ameoga
vizuri.
Basi yule bwana katika hali hiyohiyo, akaenda kwa Bi. Mkubwa. Bi. Mkubwa
akamwona mumewe katika hali ile, akasikitika sana. Akamvua nguo zenye
kinyesi, akamwosha, na kumvika nguo nyingine.
Ndipo yule bwana akamwambia mke wake, “Pete na kipande cha akili vyote
nimepata. Isipokuwa kipande cha akili nimekipata hapahapa.” Akachukua
zawadi zote, hata zile za Bi. Mdogo, akampa yule Bi. Mkubwa, na kumfukuza
Bi. Mdogo.
Wakaishi raha mustarehe.
Riwaya ya Kiswahili (Madumulla, 2009: 94 - 95)
Istiara ni hadithi ambayo maana yake ya wazi inawakilisha maana iliyofichika.
Kwa hiyo, maana huwasilishwa kwa njia ya mafumbo. Kwa mfano, hadithi
mashuhuri ya zimwi linalovamia kijiji na kuwameza wanakijiji wote isipokuwa
mwanamke mmoja mjamzito ni istiara. Katika hadithi hiyo, mama huyo mjamzito
baadaye anajifungua mtoto na kumlea akiwa mafichoni. Mtoto anapokua
anamuuliza mama yake kwa nini wako peke yao kijijini, wakazi wengine
walikwenda wapi. Mama yake anamweleza kuwa watu wote walimezwa na zimwi
ambalo linaishi katika msitu ulio karibu na kijiji hicho. Mtoto anaamua kwenda
kupambana na zimwi hilo hadi analiua. Baada ya kuliua analipasua tumbo na
kuwatoa watu wote waliomezwa wakiwa bado hai. Watu wanafurahi na kumfanya
10 Kitabu cha Mwanafunzi
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 10
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 10 23/06/2024 17:54