Page 18 - Fasihi_Kisw_F5
P. 18
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
Fasihi Simulizi
Hadithi Semi Ushairi Sanaa za maonesho
FOR ONLINE READING ONLY
Ngano Methali Nyimbo Majigambo
Tarihi Misemo Mashairi Tambiko
Visasili Mizungu Ngonjera Ngoma
Vigano Mafumbo Maghani Miviga
Soga Vitendawili Vichekesho
Ngomezi
Utani
Maigizo
Michezo ya watoto
Kielelezo namba 2.1: Tanzu na vipera vya fasihi simulizi
Yafuatayo ni maelezo ya tanzu na vipera hivyo:
Shughuli ya 2.2
Kwa kutumia vyanzo mbalimbali vya maarifa, fafanua utanzu wa hadithi na
vipera vyake.
Hadithi
Hadithi ni utungo unaotumia lugha ya mjazo (nathari) ili kueleza kisa fulani kwa
mpangilio wa matukio. Mpangilio huo hutumia wahusika ambao ndio watendaji
wa matukio hayo. Vilevile, hadithi huwa na kisa kinachofululiza tangu mwanzo
hadi mwisho ili kukamilisha muundo wake.
Hadithi huwasilishwa na msimuliaji mbele ya hadhira katika mandhari maalumu
kama vile chini ya mti mkubwa, sebuleni, darasani au uwanjani. Vilevile, huweza
kuwasilishwa kwa njia za kidijiti. Aghalabu, simulizi hufanyika katika muda
maalumu, hususani baada ya kazi. Kama inavyoonekana katika Kielelezo namba
2.1, utanzu wa hadithi una vipera vitano ambavyo ni ngano, tarihi, visasili,
vigano, na soga.
Kitabu cha Mwanafunzi 7
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 7 23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 7