Page 11 - Fasihi_Kisw_F5
P. 11
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
Dibaji
Kitabu hiki cha Fasihi ya Kiswahili: Kidato cha Tano kimeandikwa mahususi
kwa mwanafunzi wa Kidato cha Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kitabu hiki kimeandaliwa kulingana na Muhtasari wa Somo la Fasihi ya Kiswahili
FOR ONLINE READING ONLY
wa mwaka 2023 uliotolewa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia. Baadhi
ya maudhui ya kitabu hiki yamehamishwa kutoka katika Kitabu cha Kiswahili
Shule za Sekondari Kidato cha Tano na Sita cha mwaka 2019. Kitabu hicho
kiliandaliwa kulingana na Muhtasari wa Somo la Kiswahili wa mwaka 2009
uliotolewa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.
Kitabu hiki kimegawanywa katika sura sita: Dhana na chimbuko la fasihi, Fasihi
simulizi na fasihi andishi, Kutathmini kazi za kifasihi, Maadili katika fasihi,
Ujumi katika kazi za kifasihi, na Kubuni kazi changamani za kifasihi. Maudhui
ya kitabu hiki yamewasilishwa kwa njia ya matini, shughuli za kufanya, pamoja
na vielelezo ambavyo vinachochea ujenzi wa umahiri unaokusudiwa kwa kila
sura. Vilevile, katika kila sura kuna mazoezi yenye lengo la kupima na kujenga
uelewa pamoja na ujuzi katika somo hili. Hivyo basi, mwanafunzi unapaswa
kufanya mazoezi na shughuli zote zilizomo kwenye kitabu hiki pamoja na kazi
nyingine utakazopewa na mwalimu. Pia, unapaswa kuandaa mkoba wa kazi kwa
ajili ya kutunza kazi mbalimbali zinazotokana na ujifunzaji.
Jifunze zaidi kupitia Maktaba Mtandao https://ol.tie.go.tz/videos
Taasisi ya Elimu Tanzania
x Kitabu cha Mwanafunzi
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 10
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 10 23/06/2024 17:54