Page 29 - Fasihi_Kisw_F5
P. 29
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
(b) Mashairi
Mashairi ni tungo zenye kuelezea au kuonesha kwa ufupi wazo au jambo au
hisi fulani kuhusu binadamu na mazingira yake. Mambo hayo huelezwa
katika mpangilio maalumu wa maneno fasaha yenye muwala, aghalabu kwa
FOR ONLINE READING ONLY
lugha ya kitamathali yenye kugusa moyo. Tunaposema mpangilio wa maneno
tunamaanisha kuwa mpangilio wa maneno katika shairi hufuata kanuni tofauti na
ule wa nathari. Si lazima shairi kufuata kanuni za miundo ya sentensi inayotumika
katika lugha husika. Mathalani, badala ya kuandika usikate tamaa maishani
huweza kuandikwa maishani usikate tamaa - mpangilio ambao ni tofauti na
mpangilio wa kawaida. Baadhi ya tungo za taarabu ni ushairi simulizi.
Ngonjera
Ngonjera ni neno la Kigogo lenye maana ya “twende pamoja” au “tuambatane.”
Kipera hiki kilikuwapo toka zamani ila kilihuishwa mwishoni mwa miaka ya
1960 na Mathias Mnyampala katika harakati zake za kuelezea siasa ya Ujamaa
na Kujitegemea.
Ngonjera ni mazungumzo au majibizano ya kishairi kuhusu mada fulani. Kwa
kawaida, ngonjera haziimbwi, hughaniwa. Aghalabu, majibizano hayo huwa na
washiriki wa pande mbili, upande wa wanaopinga na upande wa wanaotetea hoja.
Wahusika hawa hutumia lugha ya kiishara pamoja na miondoko ya mwili kama
vile mikono, macho na midomo. Kutokana na wahusika kutumia miondoko,
ngonjera huitwa ushairi wa maigizo. Katika ngonjera, suluhisho hupatikana
mwishoni mwa majibizano, ambapo pande mbili zinazopingana hukubaliana.
Ingawa ngonjera za Mathias Mnyampala ni fasihi andishi, lakini zinaweza
kutendwa jukwaani. Mfano mzuri ni ngonjera ya Mkopo wa Fedha ya Mathias
Mnyampala inayopatikana katika kitabu cha Ngonjera za Ukuta. Ngonjera hiyo
ni majibizano ya papo kwa papo.
Mkopaji
Hodi Bwana nimekuja, nina shida na tatizi
Nijile kutaka haja, arubani ghawazi
Tazileta kwa pamoja, siku mbili zizi hizi
Tafadhali nikopeshe, haondoe shida yangu
Mkopwaji
Nimekwisha kusikia, tuliza yako nafusi
Haja nitakukidhia, Inshallah kitu hukosi
18 Kitabu cha Mwanafunzi
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 18
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 18 23/06/2024 17:54