Page 27 - Fasihi_Kisw_F5
P. 27
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
kawaida, kitendawili hupewa jibu kwa neno moja au zaidi au maelezo. Kama
ilivyo katika kazi nyingine za fasihi, vitendawili hutumika kuburudisha, kukuza
uwezo wa kufikiri, kupamba lugha, kukosoa au hata kukejeli. Tazama mifano
ifuatayo:
FOR ONLINE READING ONLY
(i) Pango langu limejaa mawe - kinywa.
(ii) Nyumba yangu ina nguzo moja - uyoga/mwavuli.
(iii) Blanketi la babu lina chawa - mbingu na nyota.
(iv) Bibi amejitwisha machicha ya nazi - mvi.
Uundaji wa vitendawili hutegemea mazingira ambako kitendawili hicho
hutumika. Tazama mifano ifuatayo:
(i) Watoto wa sultani wamevaa kofia.
(ii) Nimenunua sungura nimemvika kofia.
(iii) Nikune kichwa nikupe moto.
Jibu la vitendawili hivi vyote ni njiti ya kiberiti.
Tofauti ya vitendawili vya (i), (ii) na (iii) inatokana na mazingira. Kitendawili cha
(i) kimeundwa katika mazingira ambayo sultani aliwahi kuishi. Kitendawili cha
(ii) kimeundwa katika sehemu yenye wafugaji au pori lenye sungura. Kitendawili
cha (iii) kimeundwa katika mazingira yanayoakisi udugu, ambapo ni rahisi mtu
kuomba kukunwa kichwa.
Shughuli ya 2.4
Tumia maktaba au maktaba mtandao na vyanzo vinginevyo kujadili maana, sifa
na vipera vya ushairi simulizi.
Ushairi simulizi
Ushairi simulizi ni utanzu wa fasihi simulizi ambao huwasilishwa kwa hadhira
kwa njia ya uimbaji au ughani badala ya usemaji wa kawaida. Ushairi simulizi
ulianza wakati binadamu alipoanza kufanya kazi. Kupitia lugha, binadamu
alibuni nyimbo za kazi. Nyimbo hizo ndizo msingi wa fasihi simulizi. Nyimbo za
kazi zilitungwa kwa kuzingatia mapigo ya zana za kazi ili ziweze kukumbukwa
kwa urahisi.
16 Kitabu cha Mwanafunzi
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 16 23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 16