Page 39 - Fasihi_Kisw_F5
P. 39
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
Shughuli ya 2.8
Kwa kutumia vyanzo vya mtandaoni na maktabani eleza sifa za fasihi andishi na
tanzu zake.
FOR ONLINE READING ONLY
Tanzu na vipera vya fasihi andishi
Kama ilivyo kwa fasihi simulizi, fasihi andishi pia ina tanzu zake. Kwa mujibu
wa wataalamu mbalimbali kama vile Wamitila (2002) na Mulokozi (2017) kuna
tanzu nne za fasihi andishi ambazo ni ushairi, hadithi fupi, tamthiliya na riwaya.
Kadhalika, tanzu hizo zimegawanyika katika vipera. Tazama Kielelezo namba
2.2.
Fasihi Andishi
Ushairi Hadithi fupi Tamthiliya Riwaya
Mashairi Dhati Tanzia Dhati
Tenzi Pendwa Ramsa Pendwa
Ushairi wa maigizo Melodrama
(ushairi wa
ngonjera na ushairi Tanzia-ramsa
wa kidrama)
Kielelezo namba 2.2: Tanzu za fasihi andishi
Shughuli ya 2.9
Kwa kutumia vyanzo vya maktabani au vinginevyo, jadili dhana na chimbuko la
ushairi wa Kiswahili.
Ushairi
Mulokozi (2017) anaueleza ushairi kuwa ni “sanaa ya lugha ya mkato yenye
ubunaji inayosawiri au kueleza jambo, hisi, hali au maono kwa namna yenye
kuvutia hisia na katika mpangilio wa maneno wenye urari na wizani.” Inamaanisha
kuwa ushairi husawiri mawazo, hisi au tukio kwa muhtasari katika mpangilio
maalumu wa lugha teule ya kitamathali. Kwa hiyo, ushairi hutofautiana na tanzu
nyingine za fasihi andishi katika umbo na matumizi ya lugha. Tanzu nyingine
hutumia lugha ya mjazo ya kinathari lakini ushairi hutumia lugha ya mkato, yenye
28 Kitabu cha Mwanafunzi
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 28
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 28 23/06/2024 17:54