Page 44 - Fasihi_Kisw_F5
P. 44
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
3. Bado ungali kijana,
Na dunia ngumu sana,
Kukufunza kukuona,
FOR ONLINE READING ONLY
Ni jambo welekea.
Maisha Yangu na Baada ya miaka Hamsini (Robert, 1966: 6)
Beti za hapo juu zinaonekana wazi kuwa zimeundwa na mishororo minne. Kina
cha mshororo wa mwisho “a” ni tofauti na vina vya mishororo mingine mitatu
katika beti zote.
Ushairi wa maigizo
Huu ni utanzu mmojawapo wa ushairi wa Kiswahili. Utanzu huu tunaweza
kuuweka katika michepuo miwili ambayo ni ngonjera na ushairi wa kidrama.
(i) Ngonjera
Ngonjera ni aina ya ushairi andishi ambao huhusisha mabishano ya pande mbili.
Upande unaojua na ule usiojua jambo fulani. Kwa hiyo ushairi wa ngonjera
huandikwa kidayalojia ukihusisha pande mbili. Lengo kuu ni kuonesha udhaifu
wa hoja kinzani kwa kuzikosoa hoja hizo ili, hatimaye, hoja zilizolengwa
zionekane kuwa na ushawishi mkubwa. Tazama mfano ufuatao wa ushairi wa
beti chache za ngonjera:
Ngonjera ni kitu gani?
MDADISI
Ngonjera ni kitu gani, nasikia kila mara,
Yatamkwa midomoni, tena mbele ya hadhara,
Je, maana yake nini, nami nipate busara,
Maana yake ngonjera, nambie nami nijue.
JAWABU
Ngonjera zina kiini, cha mafunzo ya busara,
Mafunzo yenye kipini, cha kuamsha fikira,
Za mawazo akilini, na kugeuza majira,
Maana yake ngonjera, ni mafunzo kwa shairi.
Kitabu cha Mwanafunzi 33
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 33 23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 33