Page 43 - Fasihi_Kisw_F5
P. 43
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
Ukichunguza beti hizi mbili, utaona kwamba hakuna mizani linganifu wala
urari wa vina. Kilichozingatiwa ni uteuzi wa maneno wenye kujenga picha na
kumvutia msomaji au msikilizaji.
Wanausasa wanasisitiza mshairi awe na uhuru katika kutunga mashairi, na
FOR ONLINE READING ONLY
kueleza mawazo yake bila kubanwa na kanuni za wanamapokeo. Kitu cha msingi
katika shairi ni mpangilio wa maneno, lugha ya picha au taswira, tamathali za
semi, hisia za kishairi na ujumbe.
(b) Tenzi
Dhana ya tenzi imekwishaelezwa katika kipengele cha fasihi simulizi. Mambo
machache ya kuyaongezea katika kipengele hiki ni kwamba, mara nyingi, tenzi
huanza na dua, ambapo mwandishi humwomba Mungu amwongoze katika
uandishi wake. Kwa kawaida, tenzi huwa na beti nyingi kuliko shairi la kawaida,
lakini tenzi nyingi ni fupi kuliko tendi.
Beti za utenzi zinatakiwa ziwe hamsini na kuendelea. Hata hivyo, urefu wa
utenzi hutegemea uzito wa maudhui na ujuzi wa mwandishi. Aghalabu, mstari
wa utenzi huwa nusu ya mshororo wa shairi la kimapokeo. Hivyo, utenzi huwa
na mizani minane. Vilevile, vina katika mishororo mitatu ya kwanza, hufanana
lakini mshororo wa mwisho huwa na kina tofauti. Kina hiki ambacho huitwa
bahari hakibadiliki katika utenzi mzima. Tazama mfano katika baadhi ya beti za
utenzi ufuatao:
Utenzi wa hati
1. Leo nataka binti,
Ukae juu ya kiti,
Ili uandike hati,
Ndogo ya wasia.
2. Mimi kwako ni baba,
Hati hii ya huba,
Andika iwe akiba,
Asaa itakufaa.
32 Kitabu cha Mwanafunzi
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 32
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 32 23/06/2024 17:54