Page 47 - Fasihi_Kisw_F5
P. 47
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
Yameshindwa chini kuzama, kwenye kina cha urazini,
Nao wahenga vibandani, nje tena hawatoki,
Hakuna tena ngoma, ya kugeana kani,
FOR ONLINE READING ONLY
Na ushairi umehama, umerudi upeponi,
Lakini majani makavu, sasa hayatingishiki,
Nayo madirisha ya nyumba, imara yamefungwa,
Waliomo ndani wahofu, hasira ya mizimu.
Kichomi (Kezilahabi, 1988)
(i) Toa maoni yako kuhusu hoja ya kuwa ili utungo uitwe shairi,
sharti ukidhi vigezo vya kauli 1(a)
(ii) Tathmini ukweli wa kinachosemwa katika kauli (b)
ukihusianisha na hali halisi ya sasa ya ushairi wa Kiswahili.
2. Soma shairi la kisasa, kisha bainisha vipengele mbalimbali vya ushairi.
3. Soma beti ishirini (20) za utenzi uupendao kisha chambua vipengele vya
fani na maudhui.
4. Soma shairi lifuatalo, kisha jibu maswali yanayofuata.
Amina
1. Amina umejitenga, kufa umetangulia,
Kama ua umefunga, baada ya kuchanua,
Nakuombea mwanga, peponi kukubaliwa,
Mapenzi tuliyofunga, hapana wa kufungua.
2. Nilitaka unyanyuke, kwa kukuombea dua,
Sikupenda ushindike, maradhi kukuchukua,
Ila kwa rehema yake, Mungu amekuchagua,
Mapenzi tuliyofunga, hapana wa kufungua.
36 Kitabu cha Mwanafunzi
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 36
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 36 23/06/2024 17:54