Page 50 - Fasihi_Kisw_F5
P. 50
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
Hadithi fupi za kisiasa ni zile zinazohusu masuala ya kisiasa. Mifano ya hadithi
hizo ni “Wali wa Ndevu” (Ruhumbika, 1974), “Cha Mnyonge Utakitapika
Hadharani”, “Magwanda Kubilya na Vyama Vingi” na “Mayai Waziri wa
Maradhi” (Kezilahabi katika Msokile, 1992).
FOR ONLINE READING ONLY
Hadithi fupi za kiutamaduni zinahusu masuala ya mila na desturi. Mifano ya
hadithi fupi za kundi hili ni Tamaa Mbele (Banzi, 1970) na “Siku ya Mganga”
(Mpilipili, katika Wamitila, 2012).
Hadithi fupi za kifalsafa huzungumzia tafakuri kuhusu masuala mazito
yanayomzunguka mwanadamu na ulimwengu wake. Mifano ya hadithi
fupi za kifalsafa ni “Wasubiri Kifo” (Kezilahabi, katika Msokile, 1992) na
“Mchakamchaka wa Maisha” (katika Komba, 1978).
Hadithi fupi pendwa ni zile ambazo huzungumzia masuala yanayosisimua kama
vile mapenzi, matukio yenye uajabu ajabu, mauaji na upelelezi. Mifano ya hadithi
hizi ni “Sadiki Ukipenda” (Mohamed, 2002)
Pamoja na uainishaji wa hadithi fupi uliofanywa hapo juu, ni vigumu kuwa
na hadithi fupi yenye maudhui ya mwelekeo mmoja. Hivyo, hadithi fupi moja
inaweza kubeba maudhui ya aina mbalimbali.
Shughuli ya 2.11
Kwa kutumia vyanzo mbalimbali, soma hadithi fupi zisizopungua nne (4) kisha,
bainisha aina zake na chambua maudhui ya hadithi hizo.
Shughuli ya 2.12
Kwa kutumia vyanzo mbalimbali, fafanua dhana na historia ya tamthiliya.
Tamthiliya
Tamthiliya ni mchezo ulioandikwa ili utendwe jukwaani au usomwe, kwa
malengo mbalimbali. Tamthiliya hujengwa na wahusika na migogoro iliyomo
katika mchezo. Migogoro ndiyo hukuza mwendo wa tamthiliya kwa kutumia
visa ambavyo hutendwa na wahusika mbalimbali. Wahusika huzungumza na
kutenda matendo mbalimbali kisanii.
Historia ya tamthiliya
Tamthiliya haikuwapo nchini Tanzania kabla ya ujio wa Waingereza. Ujio wao
ulileta drama ambayo ndiyo chanzo cha tamthiliya. Drama iliingizwa shuleni na
Waingereza kwa lengo la kuwaburudisha na kuwakumbusha utamaduni wao, hasa
Kitabu cha Mwanafunzi 39
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 39 23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 39