Page 51 - Fasihi_Kisw_F5
P. 51
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
baada ya saa za kazi ambapo wengi wa walimu walikuwa Waingereza. Ilikuwa
rahisi kuanzisha vikundi vya drama shuleni kwa sababu shule nyingi zilikuwa za
bweni; na hivyo, wanafunzi walipatikana muda wote. Vilevile, wanafunzi hao
walifahamu vizuri lugha ya Kiingereza. Tamthiliya nyingi zilizoigizwa ni zile
FOR ONLINE READING ONLY
zilizoandikwa na Waingereza. Miongoni mwa tamthiliya hizo ni The Merchant
of Venice (Shakespeare, 1596) na Julius Caesar (Shakespeare, 1599). (Kwa kuwa
tamthiliya hizi hazikuwa na uhusiano na mazingira ya Kitanzania, Watanzania
walioziigiza waliona ni kiburudisho tu yaani tamthiliya hizo hazikuwa na maana
kubwa kwao. Kadiri muda ulivyopita, baadhi ya Watanzania walivutika na sanaa
ya tamthiliya. Hata hivyo, hawakuwa na ujuzi wa kuandika tamthiliya kama zile
za Waingereza. Miaka ya mwanzo baada ya uhuru, maudhui hayakubadilika
mpaka lilipotangazwa Azimio la Arusha mwaka 1967. Maudhui ya tamthiliya
ya baada ya Azimio la Arusha yalichukua sura mpya kwa kutangaza siasa ya
Ujamaa na Kujitegemea kwa kuunga mkono au kukosoa.
Tamthiliya za mwanzo ziliathiriwa sana na vichekesho. Pia, ziliathiriwa na
tamthiliya za Kiingereza. Watunzi walitunga tamthiliya zilizofanana kimaudhui
na zile za akina Shakespeare. Kwa mujibu wa Mazrui (2007) na Mulokozi
(2017), tamthiliya za mwanzo za Kiswahili zilitungwa nchini Kenya. Mifano ya
tamthiliya hizo ni Mgeni Karibu (Hyslop, 1957), Nakupenda Lakini (Kuria, 1957)
na Nimelogwa Nisiwe na Mpenzi (Ngugi, 1961). Kwa upande wa Tanzania, miaka
ya 1960, tamthiliya za Kiingereza zilitafsiriwa. Miongoni mwa tamthiliya hizo
ni zile za Shakespeare za Juliasi Kaisari (Nyerere, 1964), Mabepari wa Venisi
(Nyerere, 1969), Tufani (Mushi, 1969) na tamthiliya ya Kiyunani ya Mfalme
Edipode (Mushi, 1969). Tamthiliya nyingine ni zile zilizoandikwa na Waafrika.
Zilizotafsiriwa ni Mtawa Mweusi (wa Thiong’o, 1970), Masaibu ya Ndugu Jero
(Yahaya, 1974) na Nitaolewa Nikipenda (wa Thiong’o na wa Mirii, 1982).
Kuanzia miaka ya 1960, watunzi wa Kitanzania walianza kutunga tamthiliya
za Kiswahili kwa ajili ya Watanzania. Miongoni mwa watunzi waliojitokeza ni
Ebrahim Husein ambaye tamthiliya yake ya kwanza ni, Wakati Ukuta (1967),
ilishinda na kupata tuzo katika mashindano. Tamthiliya nyingi zilizotungwa
miaka ya 1960 ziliigizwa tu shuleni na katika kumbi za maonesho lakini
hazikuchapishwa.
Tamthiliya nyingi za Kiswahili zilichapishwa kama matokeo ya kuhitimu kwa watu
wengi katika fani ya sanaa za maonesho katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Pia, yalikuwa ni matokeo ya kuanzishwa kwa mashindano ya uigizaji miaka
ya 1970 - 1990. Baadhi ya tamthiliya zilizochapishwa ni Kinjekitile (Hussein,
40 Kitabu cha Mwanafunzi
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 40 23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 40