Page 56 - Fasihi_Kisw_F5
P. 56
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
Historia ya riwaya
Riwaya ni utanzu wa hivi karibuni zaidi ukilinganishwa na ushairi na tamthiliya.
Inadaiwa kwamba riwaya ilipata umbo ililonalo hivi sasa katika karne ya 18
huko Ulaya. Riwaya ilizuka kutokana na maendeleo na mageuzi ya kiutamaduni
FOR ONLINE READING ONLY
na viwanda. Ukoloni na “uvumbuzi” viliumba hali zilizohitaji kuelezwa
kwa mawanda mapana kuliko ilivyowezekana katika ngano na hadithi fupi.
Uchangamani wa maisha katika nyanja mbalimbali kama vile siasa, utamaduni
na uchumi ulihitaji kuwa na utanzu wa fasihi ulio na uchangamani kifani na
kimaudhui pia. Kupanuka kwa usomaji, hasa wakati wa mapinduzi ya viwanda
huko Uingereza, kuliwafanya waandishi waandike kazi ndefu kwa sababu
walikuwapo wasomaji, hasa wanawake, waliokuwa wakibaki majumbani wakati
waume zao wakiwa viwandani (Senkoro, 1984; Njogu na Chimerah, 1999;
Madumulla, 2009).
Afrika ni miongoni mwa mabara yenye historia fupi zaidi ya riwaya, ambapo
maandiko ya riwaya yalianza kujitokeza mwishoni mwa karne ya 19. Katika eneo
la Afrika ya Mashariki, kazi za kinathari za kwanza hazikukidhi ubora wa usanii
na ubunifu. Baadhi ya maandiko ya awali ni Habari za Wakilindi (el Ajjemi, 1885,
1907, 1962), Tulivyoona na Tulivyofanya Uingereza (Kayamba, 1933), Mwaka
katika Minyororo (Sehoza, 1921) na Uhuru wa Watumwa (Mbotela, 1934). Vyote
hivi vinaangukia katika kundi linaloendana na tawasifu au masimulizi ya wasafiri.
Kwa hakika, kiwango cha usanifu wa vitabu hivi ni cha chini.
Nchini Tanzania, kama ilivyo kwa nchi nyingine zinazoendelea, nathari andishi
ya kibunifu ni fani ambayo ilichelewa kuja. Nathari bunifu simulizi, kama vile
hadithi, hekaya na ngano zilizosimuliwa kwa mdomo ndizo ambazo zilizotawala
ndani ya jamii.
Kwa upande wa fasihi andishi, kwa kipindi kirefu, maandiko ya fani ya ushairi,
hususani tenzi za Kiswahili katika hati ya Kiarabu, ndiyo yaliyotamba katika eneo
la Pwani ya Afrika ya Mashariki. Maandiko ya kinathari yalianza baada ya ujio
wa wamisionari. Nathari simulizi inayojulikana kuandikwa na wenyeji ni Habari
za Muma (bin Hemed, 1880), nayo ilichapishwa mwaka 1935 katika Mambo
Leo, gazeti la Kiswahili lililovuma wakati wa ukoloni wa Waingereza. Nathari
nyingine ni ile ya Habari za Wakilindi iliyoandikwa na Abdallah bin Hemed bin
Ali el Ajjemy mzaliwa wa Zanzibar kwa baba wa Kiarabu na mama wa Kihehe,
na ambayo juzuu ya kwanza ilichapishwa mwaka 1894, ya pili mwaka 1904 na ya
tatu mwaka 1907. Kitabu hiki kilihusu masimulizi ya Wasambaa. Kumbukumbu
nyingine ni zile zilizohusu Lamu na ambazo zinasadikiwa kuwa ziliandikwa
Kitabu cha Mwanafunzi 45
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 45 23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 45