Page 55 - Fasihi_Kisw_F5
P. 55
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
Sifa za riwaya
Kuna sifa mbalimbali za riwaya. Kwa kawaida riwaya huwa:
(a) ndefu ikilinganishwa na tanzu nyingine. Urefu wa riwaya ya Mungu
Hakopeshwi (Baharoon, 2021) kwa mfano, ni tofauti na ule wa hadithi fupi
FOR ONLINE READING ONLY
ya Uwike Usiwike Kutakucha (Ruhumbika, 1978);
(b) na visa changamani, yaani huwa na visa zaidi ya kimoja, ambapo kisa kikuu
hujengwa na visa vidogo;
(c) na wahusika wengi na waliokuzwa. Kutokana na riwaya kuwa na visa vingi,
basi huwa na wahusika wengi ambao humwezesha mwandishi kukidhi haja
hii;
(d) na mandhari pana na huendelezwa kikamilifu. Kwa kuwa riwaya
hushughulikia mawazo mengi, hujishughulisha na vipengele vingi vya
maisha ambavyo hupatikana katika nyakati na mahali tofauti kama vile
shuleni, mijini, vijijini, nyumbani na barabarani. Ili kushughulikia mazingira
mapana, simulizi hutumia kipindi kirefu cha wakati ikilinganishwa na
kazi kama vile za hadithi fupi ambazo huweza kuchukua kipindi kifupi tu
kukamilika;
(e) na migogoro iliyokuzwa zaidi kwa sababu mwandishi ana uhuru mkubwa
wa kuiibua na kuieleza kwa kina;
(f) Hutumia lugha ya kisanii ya kinathari / lugha ya mjazo; na
(g) Kwa sababu ya urefu na upana wake, riwaya huwa na uwezo wa kubeba au
kutomelea tanzu nyingine (kama vile barua, insha, shairi, wimbo au igizo)
bila matatizo. Mathalani, katika riwaya ya Kiu ya Haki (Mwanga,1983)
mwandishi ametumia hadithi ndani ya hadithi. Hadithi mojawapo ni ile ya
Mzee Fundisha anayesimulia yaliyompata alipovamiwa na polisi nyumbani
kwake na kulazimishwa kutoa rushwa ya Sh. 2,000 ingawa hakuwa na
hatia. Vilevile, kuna hadithi ya Sikujua, anayesimulia yaliyompata miaka
kumi iliyopita wakati yeye na Pondamali wakifanya biashara ya kubadilisha
fedha.
44 Kitabu cha Mwanafunzi
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 44 23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 44