Page 59 - Fasihi_Kisw_F5
P. 59
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
ni Nyota ya Huzuni (Liwenga, 1978), Njozi Iliyopotea (Mung’ong’o, 1979), Sudi
ya Yohana (Chachage, 1981), Kivuli (Chachage, 1981), Harusi (Safari, 1984) na
Miradi Bubu ya Wazalendo (Ruhumbika, 1992).
Riwaya hizo za kihakiki zimeendelea kuandikwa mpaka miaka ya 2000. Riwaya
FOR ONLINE READING ONLY
hizi zimejadili upokezi na athari za soko huria lililotokana na sera za ubinafsishaji.
Katika mfumo huu, njia kuu za uchumi zinamilikiwa na watu binafsi, wengi
wao wakiwa si wazawa. Kwa hiyo, wazawa wameendelea kuishi maisha
magumu kinyume na matarajio waliyokuwa nayo, baada ya uhuru, hususani
baada ya kutangazwa kwa Azimio la Arusha. Mifano ya riwaya zenye maudhui
yanayohusiana na ubinafsishaji na soko huria ni Almasi za Bandia (Chachage,
1991) na Makuadi wa Soko Huria (Chachage, 2002).
Ikumbukwe kwamba hakuna mpaka bayana katika vipindi vilivyotajwa hapo juu.
Kuna kazi za fasihi andishi zenye maudhui yanayohusu vipindi tofauti katika
kipindi kimoja. Hivyo, si ajabu kukuta riwaya za kiuhakiki katika kipindi cha
Azimio la Arusha; vivyo hivyo, riwaya pendwa zinajitokeza katika vipindi vyote.
Pia, hali hii inaweza ikatokana na mhamo wa kutoka kipindi kimoja kwenda kipindi
kingine. Katika kipindi cha mpito, kunakuwa na kazi za fasihi zinazozungumzia
kipindi ambacho kinaelekea kufikia mwisho na nyingine zinakuwa na maudhui
ya kipindi kilichopo au hata kijacho.
Aina za riwaya
Riwaya hugawanywa kwa kuzingatia vigezo mbalimbali. Vigezo vilivyo maarufu
ni vya kutazama fani na maudhui. Kifani, riwaya huainishwa kwa kuzingatia
jinsi vipengele vya fani vinavyojitokeza. Kadhalika, kimaudhui, mgawanyo
hutazama mambo yanayoongelewa katika riwaya inayohusika. Kigezo hiki cha
maudhui ndicho kinachotumika katika kitabu hiki. Kwa kutumia kigezo hiki,
kuna makundi makubwa mawili ya riwaya: riwaya dhati na riwaya pendwa.
1. Riwaya dhati
Riwaya dhati ni zile zinazochambua matatizo au masuala mazito ya kijamii,
kutafuta sababu zake, athari zake na ikiwezekana ufumbuzi wake. Riwaya hizi
hukusudiwa kumfikirisha msomaji kuhusu masuala mazito na si kumstarehesha
tu. Riwaya dhati zimegawanyika katika aina mbalimbali. Aina hizo ni: riwaya
za kijamii, kisaikolojia, sira, kiistiara, kingano, teti, chuku, kihistoria, kimaadili,
kimapinduzi na kifalsafa. Pia, kuna riwaya za barua, vitisho na za watoto na
vijalunga.
48 Kitabu cha Mwanafunzi
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 48 23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 48