Page 46 - Fasihi_Kisw_F5
P. 46
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
Mfalme: Mwenzako lakini kakukosa nini?
Mwenzako kakufanya nini?
Mimi bado sijaamini
FOR ONLINE READING ONLY
Kwa kweli baya mimi sijalibaini
Basi jambo hilo lanikata maini
Na kunivunjia matumaini
Mbona unaivunja ihsani
Yake sisi tul’omwamini
0Posa za Bikisiwa (Mohamed, 2013)
Kwa jumla, kuna sifa mbalimbali za kisanaa zinazoutofautisha ushairi na tanzu
nyingine za riwaya pamoja na tamthiliya.
Zoezi la 2.2
1. Soma kauli hizi mbili kisha jibu maswali (a) na (b) yanayofuata:
(a) “Katika kitabu hiki, tungo za Euphrase Kezilahabi, Kulikoyela
Kahigi, Mulokozi na wengineo watungao tungo tutumbi zisizokuwa
na sanaa yoyote nimezitupa pembeni … Muundo wa mashairi yote
yaliyomo kitabuni humu ni ya asili ya Kibantu. Kila utungo wa
shairi umefungika upande wa mistari; umefungika upande wa vina;
ni lazima mistari iwe na vina; umefungika upande wa mizani; ni
lazima kila mstari uwe na idadi sawa ya mizani. Mashairi yote
yaimbwe; yaweza pia kusomwa au kusemwa tu. Tungo zisizotimiza
yote hayo si mashairi.”
Mgogoro wa Ushairi na Diwani ya Mayoka (Mayoka, 1986)
(b) Washairi wa mapokeo, sasa wacheza lala salama,
Katika mionzi hafifu, ya jua machweoni,
Na mahadhi yagaagaa, juu ya bahari ya utenzi,
Kitabu cha Mwanafunzi 35
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 35 23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 35