Page 49 - Fasihi_Kisw_F5
P. 49
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
Swahili Tales as Told by the Natives of Zanzibar (1870), Hekaya za Abunuwasi
(1928) na Alfu Lela Ulela (1928). Hadithi hizi zilikuwa za kimapokeo na zenye
kuingiliana na fasihi simulizi. Visa halisi vya kwanza katika hadithi za lugha
ya Kiswahili vilianza miaka ya 1950 katika magazeti ya Mamboleo, Mwafrika,
FOR ONLINE READING ONLY
Baraza, Nyota Afrika na Kiongozi. Katika miaka ya 1960, visa hivi vilianza
kuchapishwa kwenye vitabu. Baadhi ya watunzi mashuhuri wa hadithi fupi za
Kiswahili ni Gabriel Ruhumbika, Alex Banzi, Joseph Kiimbila, Kyallo Wamitila
na Owen Onyango. Baadhi ya mikusanyiko ya hadithi fupi iliyochapishwa ni
Misingi ya Hadithi Fupi (Msokile, 1992), Mwendawazimu na Hadithi Nyingine
(Mbatiah, 2000), Mimba Ingali Mimba na Hadithi Nyingine, (MacOnyango,
2006), Mizungu ya Manabii na Hadithi nyingine (Habwe, 2010), Shingo ya
Mbunge na Hadithi Nyingine (Wamitila, 2010)
Sifa za hadithi fupi
Hadithi fupi huwa na sifa au kaida zinazoitofautisha na riwaya. Nazo ni kuwa na:
(i) urefu wa kusomeka kwa mkao mmoja. Kwa kawaida hadithi fupi haizidi
maneno 10,000;
(ii) muundo sahili;
(iii) wahusika wachache ambapo, aghalabu, mhusika mkuu huwa mmoja
au wawili. Wahusika hawa hawakui kitabia wala hawakui kulingana na
maendeleo ya kisa;
(iv) dhamira chache ikilinganishwa na riwaya. Mara nyingi, huwa na dhamira
kuu moja katika kisa kikuu kimoja; na
(v) mawanda finyu ya kiwakati na kijiografia.
Aina za hadithi fupi
Hadithi fupi huainishwa katika makundi mawili: hadithi fupi dhati na hadithi
fupi pendwa. Hadithi fupi dhati huwekwa katika makundi yafuatayo: hadithi fupi
za kijamii, kisiasa, kiutamaduni na kifalsafa.
Hadithi fupi za kijamii huzungumzia masuala mbalimbali ya kijamii kama vile
ndoa, jinsia, mapenzi na malezi. Mifano ya hadithi fupi za kijamii ni: “Uwike
Usiwike Kutakucha” (Ruhumbika), na “Siri ya Bwanyenye” (Mulokozi) zote
hizi zimo katika Msokile (1992). Nyingine ni “Damu Nyeusi” (Walibora, 2007)
na “Kijana Yule” (Mohamed, 2010).
38 Kitabu cha Mwanafunzi
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 38 23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 38