Page 68 - Fasihi_Kisw_F5
P. 68

Fasihi ya Kiswahili  kwa Shule za Sekondari




               5.   Uhifadhi      Huhifadhiwa kichwani na     Huhifadhiwa katika nyaraka
                                  kuendelezwa kwa njia ya     au kwa njia za kidijiti.
                                  kupokezana, ijapokuwa
                                  kutokana na maendeleo
          FOR ONLINE READING ONLY
                                  ya teknolojia, huweza
                                  kuhifadhiwa katika vinasa
                                  sauti, kompyuta na hata
                                  maandishi.
               6.   Tanzu na      Idadi ya tanzu na vipera vya  Idadi ya tanzu na vipera
                    vipera        fasihi simulizi ni kubwa    vya fasihi andishi ni ndogo.
                                  kuliko ilivyo katika fasihi   Aidha, vipera vyake havina
                                  andishi. Aidha, huwa na     mwingiliano mkubwa.
                                  mwingiliano mkubwa wa
                                  vipera.
               7.   Mabadiliko    Hubadilika kwa haraka       Haibadiliki kwa haraka kwa
                                  kutegemeana na mahitaji ya  sababu ipo katika hali ya
                                  hadhira, tukio la kijamii na  kudumu.
                                  wakati.
               8.   Hadhira       Hadhira yake ni hai ambayo  Ni wasomaji; hivyo
                                  hushiriki katika utendaji   hawashiriki katika utendaji,
                                  kama kuitikia, kupiga       isipokuwa katika tanzu
                                  vigelegele na makofi.       chache zinazowasilishwa
                                                              kiutendaji kama vile
                                                              mashairi na tamthiliya.
               9.   Wahusika      Hutumia wahusika            Hutumia zaidi wahusika
                                  mchanganyiko (kwa mfano  binadamu. Wahusika wasio
                                  binadamu, wanyama, mimea  binadamu hutumika mara
                                  na vitu visivyo na uhai).   chache.
               10.  Muundo        Huwa na muundo wa moja      Huweza kuwa na muundo
                                  kwa moja, aghalabu bila     wa moja kwa moja au
                                  utata.                      changamani kutegemeana na
                                                              utanzu.

               Shughuli ya 2.16
              Kwa kutumia vyanzo vya maktabani na mtandaoni, eleza namna fasihi simulizi
              ilivyochangia kupatikana kwa fasihi andishi.







                     Kitabu cha Mwanafunzi                                            57
                        Kidato cha Tano



                                                                                            23/06/2024   17:54
     FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd   57                    23/06/2024   17:54
     FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd   57
   63   64   65   66   67   68   69   70   71   72   73