Page 77 - Fasihi_Kisw_F5
P. 77
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
Fani hufumbata maudhui; na maudhui ndiyo huitengeneza au kuipa umbo
fani. Inamaanisha kuwa ili kazi ya fasihi ikamilike na iwe bora, lazima iwe na
vipengele vya fani na maudhui ambavyo huhitajiana, hushirikiana, hutegemeana,
huwiana na hukamilishana. Uwiano na ushirikiano wa fani na maudhui ndio
FOR ONLINE READING ONLY
unaokamilisha kazi ya fasihi.
Shughuli ya 3.2
(a) Chambua vipengele vya fani na maudhui katika hadithi teule moja
uliyosoma kisha jibu maswali yafuatayo.
(i) Ni kwa namna gani wahusika wa hadithi hiyo wanahusiana na
migogoro iliyojitokeza?
(ii) Kwa nini mwandishi ametumia muundo alioutumia katika kufikisha
ujumbe wake?
(iii) Ni kwa namna gani lugha iliyotumika inachangia kuibua maudhui
katika hadithi hiyo?
(iv) Taswira alizozitumia mwandishi zina mchango gani katika kuelewa
dhamira za hadithi hii?
(v) Mtindo wa uandishi wa hadithi hiyo umechangiaje katika kuwasilisha
maudhui?
(b) Chambua uhusiano wa fani na maudhui katika kazi yoyote ya fasihi ya
Kiswahili.
Uhusiano wa fani na maudhui katika kazi za fasihi
Mwandishi na mhakiki wa kazi za fasihi anapaswa/hupaswa kuzingatia uhusiano
wa vipengele vya fani na maudhui katika kubuni na kuchambua kazi. Endapo
mwandishi na mhakiki huyo hatazingatia na kuhusianisha ipasavyo vipengele
hivyo, vya fasihi uhakiki wake utakuwa chapwa.
Shughuli ya 3.3
Kwa kutumia mifano, jadili umuhimu wa fani na maudhui katika kazi za fasihi.
Dhima za vipengele vya fani na maudhui katika kazi za fasihi
Vipengele vya fani na maudhui vina dhima kubwa katika kazi ya fasihi. Dhima
hizo muhimu zinaweza kuelezwa kama ifuatavyo:
66 Kitabu cha Mwanafunzi
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 66
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 66 23/06/2024 17:54