Page 80 - Fasihi_Kisw_F5
P. 80
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
(iii) kumsaidia mhakiki kugundua jambo jipya au kuliboresha lililokuwapo
awali.
Uchambuzi wa nadharia teule za uhakiki wa kazi za fasihi
FOR ONLINE READING ONLY
Shughuli ya 3.5
Kwa kutumia vyanzo vya mtandaoni au maktabani, taja nadharia nne (4) za
uhakiki wa kazi za fasihi.
Shughuli ya 3.6
Kwa kutumia vyanzo vya mtandaoni au maktabani, fafanua maana na misingi ya
nadharia ya umuundo katika kuhakiki kazi za fasihi.
Nadharia ya umuundo
Umuundo ni nadharia ya uhakiki wa fasihi iliyojikita kwenye taratibu zilizopo
katika uundwaji wa kazi ya kifasihi. Miongoni mwa waasisi wa nadharia hii
ni Ferdinand de Saussure (1857-1913) aliyeanzisha umuundo wa kiisimu.
Wanamuundo wanaeleza kuwa lugha ni mfumo wa ishara nasibu, na kwamba
kila kipengele kinahusiana na vipengele vingine katika mfumo huo. Kama ilivyo
katika mfumo wa lugha, fasihi nayo imeundwa na vipengele vinavyotegemeana.
Katika kazi ya fasihi kuna vipengele vya kisanaa vinavyojidhihirisha katika fani na
maudhui. Vipengele hivyo huelezwa kwa kutegemeana, kwani hakuna kipengele
kinachoweza kusimama peke yake bila kuhusishwa na kingine. Nadharia
ya umuundo huonesha namna vipengele vya kazi ya fasihi vinavyohusiana
na kufungamana hadi kuikamilisha kazi husika. Kwa jumla, wanaumuundo
wanaeleza kuwa kazi ya fasihi haina urejelezi wa nje bali huonwa kama mfumo
unaojitosheleza.
Misingi ya nadharia ya umuundo
Misingi mikuu ya nadharia ya umuundo ni:
(i) lugha hutawaliwa na mfumo wa ishara, ambapo vipengele vinavyounda
mfumo huo huweza kueleweka tu kwa kuangalia uhusiano wake na
vipengele vingine katika mfumo huo wa lugha badala ya kuangalia nje ya
mfumo wa lugha husika;
(ii) maana ya fasihi imejificha ndani ya mfumo wa lugha;
(iii) ishara haielezi wala haitoi uhusiano baina ya neno na kitu, bali ni
muunganiko changamani kati ya dhana iliyopo akilini na ruwaza za sauti
zinazoendana na dhana hiyo; na
Kitabu cha Mwanafunzi 69
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 69 23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 69