Page 81 - Fasihi_Kisw_F5
P. 81
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
Katika kuchambua kazi ya fasihi kwa kutumia nadharia ya umuundo, unatakiwa
kuchunguza matumizi ya lugha, na uhusiano wa vipengele vya lugha katika
kutoa maana ya kazi hiyo. Pia, chunguza namna wahusika wanavyoitumia
lugha kufikisha ujumbe uliokusudiwa. Vilevile, chunguza jinsi taswira na ishara
FOR ONLINE READING ONLY
mbalimbali zilivyotumika kujenga maana ya kazi hiyo ya fasihi. Kadhalika,
fafanua mpangilio wa vipengele vya kazi hiyo. Mathalani, iwapo unachambua
shairi zingatia namna vina, mizani, vibwagizo, beti, na mpangilio kwa jumla
vinavyosaidia kupatikana kwa maana ya shairi.
Shughuli ya 3.7
Kwa kutumia vyanzo vya mtandaoni au maktabani, fafanua maana na misingi ya
nadharia ya umaksi katika kuhakiki kazi za fasihi.
Nadharia ya umaksi
Umaksi ni nadharia inayozungumzia harakati za mwanadamu katika kupambana
na utabaka uliomo katika jamii yake. Harakati hizo huhusiana na masuala ya
uchumi, historia, siasa, jamii na mapinduzi, ambapo tabaka linalodhibiti njia kuu
za uzalishaji mali huitawala na kuidhibiti jamii. Nadharia hii iliasisiwa na Karl
Marx (1818 - 1883) na Friedrich Engels (1820 - 1895) kupitia kazi zao za Das
Kapital (1867) na Communist Manifesto (1848). Jambo kubwa katika nadharia
hii siyo kuufasili ulimwengu tu, bali kuubadilisha. Kwa mujibu wa Karl Marx,
tabaka moja hutoweka na lingine huchipuka kwa sababu ya mgongano unaotokea
kati ya tabaka tawala na tabaka tawaliwa. Mgongano huo hutokea kwa sababu
kila mara kuna tabaka la wanyonyaji na wanyonywaji.
Kwa jumla, nadharia ya umaksi huhusisha kazi za fasihi na uhalisi wa kijamii wa
wakati kazi hizo zilipotungwa. Vilevile, nadharia hii huzingatia zaidi maudhui
katika uhakiki wa kazi za kifasihi huku ikijikita katika kuhakiki maadili na njia
za kuyaboresha maisha.
Misingi ya nadharia ya umaksi
Nadharia ya umaksi ina misingi mbalimbali inayotumika katika uhakiki wa kazi
za kifasihi. Misingi hiyo ni:
(i) kutumia historia ya binadamu kuakisi harakati za kitabaka
zinazoendelea katika jamii;
(ii) kuvunjiliwa mbali kwa ubepari kama njia ya uzalishaji mali kutokana
na jitihada mbalimbali za kitabaka za kuuangamiza;
70 Kitabu cha Mwanafunzi
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 70
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 70 23/06/2024 17:54