Page 83 - Fasihi_Kisw_F5
P. 83
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
Steady (1981) ni miongoni mwa waasisi wa nadharia ya ufeministi wa Kiafrika.
Huyu alitumia nadharia hii kubainisha dhuluma zilizokuwa zikimkandamiza
mwanamke wa Kiafrika kama vile kutokuwa na uhuru wa kuchagua kuwa mzazi
kwa wakati gani au kujichagulia mume; ukeketaji wa mwanamke, unyamavu
FOR ONLINE READING ONLY
wa kulazimishwa, urithi wa mali, mila za kurithiwa, rangi yake mwenyewe na
kubaguliwa kwa mwamwake tasa.
Katika kutahadharisha kuhusu ufeministi, Badru (2019) anaeleza kuwa tangu
kuanza kwa mawazo ya ufeministi ulimwenguni msisitizo mkubwa umekuwa
ni namna gani wanawake wanaweza kujikomboa kwa kubadilisha mfumo-dume
na kupata haki na wajibu sawa. Pamoja na hatua kubwa iliyopigwa, mapigano
haya hayawezi kufanikiwa iwapo yatakuwa mapigano ya wanawake dhidi ya
wanaume. Iwapo mwanaume ataachwa nyuma na asikombolewe kutoka katika
ufungwa wa kifikra, kiutamaduni na kiuchumi alimofungwa hakuna namna
ambavyo mapambano haya yatafanikiwa.
Ni vizuri kujua kuwa nadharia ya ufeministi wa Kiafrika hainuii kuleta mgogoro
na mvutano wa nafasi mbalimbali baina ya mwanamume na mwanamke katika
jamii; bali unalenga kuamsha uelewa na usawa baina yao.
Misingi ya nadharia ya ufeministi
Ifuatayo ni misingi ya nadharia ya ufeministi ni:
(i) kukuza na kuendeleza umoja wa wanawake kupitia majukwaa mbalimbali;
(ii) kuleta usawa wa kijinsia katika maeneo mbalimbali kama malezi na
mgawanyo wa majukumu;
(iii) kumpa mwanamke uhuru na nguvu ya kufanya maamuzi katika jamii;
(iv) kuelezea kwa undani hali ya mwanamke ili kumsaidia mtu yeyote kuielewa
hali hiyo;
(v) kumpa mwanamke haki ya kushirikishwa na kushiriki katika masuala
mbalimbali ya jamii;
(vi) kuhimiza mhusika wa kike katika kazi za fasihi awe mfano mzuri wa kuigwa
katika jamii;
(vii) kutambua na kuthamini kazi za fasihi zilizotungwa na wanawake; na
(viii) kuepuka usaguzi wa kimapokeo uliojengewa misingi ya kiimani na wenye
mawazo hasi kuhusu nafasi ya mwanamke katika jamii.
72 Kitabu cha Mwanafunzi
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 72 23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 72