Page 84 - Fasihi_Kisw_F5
P. 84
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
Kwa hiyo, unapohakiki kazi ya fasihi kwa kutumia nadharia ya ufeministi,
unatakiwa kuchambua masuala yanayohusiana na usawa wa kijinsia kati ya
mwanamke na mwanamume katika nyanja za kiutamaduni, kidini, kijamii,
kisiasa, na kiuchumi.
FOR ONLINE READING ONLY
Shughuli ya 3.9
Kwa kutumia vyanzo vya mtandaoni na maktabani, fafanua maana na misingi ya
nadharia ya uhalisia katika kuhakiki kazi za fasihi.
Nadharia ya uhalisia
Nadharia ya uhalisia inahusu kusawiri na kuakisi maisha ya mwanadamu na
mazingira. Nadharia hii inaepuka masuala ya unjozi na huyaelezea maisha kwa
uyakinifu kama yalivyo katika jamii. Waasisi wa nadharia hii ni: George Wilhelm
Hegel (1770-1831), Friedrich Schiller (1759-1805), na Gustave Flaubert (1821-
1880). Nadharia hii husisitiza kuwa kazi ya sanaa ioneshe maisha ya binadamu
jinsi yalivyo. Kimsingi, nadharia hii inaichukulia kazi ya fasihi kama kioo
kinachoonesha masuala mbalimbali yanayohusiana na maisha ya binadamu.
Misingi ya nadharia ya uhalisia
Ifuatayo ni misingi ya nadharia ya uhalisia ni:
(i) uwasilishaji wa maudhui ya kazi ya fasihi uzingatie hali halisi ya jamii;
(ii) mandhari ya kazi ya fasihi yaakisi mazingira halisi;
(iii) wahusika wasawiriwe kiyakinifu ili kuakisi maisha ya kila siku;
(iv) matukio katika kazi ya fasihi yaakisi mambo kama yalivyo kisiasa, kiuchumi,
na kutamaduni na kijamii;
(v) changamoto za kijamii zitatuliwe kwa njia zinazothibitika kisayansi; na
(vi) lugha inayotumika kwenye kazi za fasihi iwe ile inayoeleweka kwa msomaji/
hadhira lengwa.
Unapohakiki kazi ya fasihi kwa kutumia nadharia ya uhalisia, unatakiwa
kuchunguza namna mwandishi alivyowaumba na kuwasawiri wahusika,
matumizi ya lugha ya kawaida, namna matukio yanavyoakisi hali halisi, na
jinsi mandhari ilivyochorwa. Vilevile, hakiki namna maudhui ya kazi hiyo
yanavyoakisi hali halisi na ukweli wa maisha ya jamii husika.
Kitabu cha Mwanafunzi 73
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 73 23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 73