Page 89 - Fasihi_Kisw_F5
P. 89
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
3. Linganisha nadharia za umuundo na umaksi zinavyotumika katika
uchambuzi wa kazi za fasihi.
4. Fafanua tofauti zilizopo kati ya nadharia ya mwingilianomatini na
mwitiko wa msomaji.
FOR ONLINE READING ONLY
5. Eleza tofauti zilizopo kati ya nadharia ya ufeministi na uhalisia.
6. Mhakiki hana nafasi katika kazi za fasihi. Jadili.
7. Kwa kutumia mifano, fafanua mitazamo kuhusu mhakiki wa kazi ya
fasihi kisha toa maoni yako.
Kuhakiki maigizo, mashairi, na tamthiliya kwa kutumia nadharia za kifasihi
Uchambuzi wa kazi za fasihi kwa kutumia nadharia za kifasihi huzingatia misingi
ya uhakiki ya nadharia husika. Hivyo, mhakiki anapaswa kuzingatia misingi ya
kila nadharia katika kuhakiki kazi za kifasihi. Ufuatao ni ufafanuzi wa namna ya
kuhakiki maigizo, mashairi na tamthiliya kwa kutumia nadharia za kifasihi.
Kuhakiki maigizo kwa kutumia nadharia za kifasihi
Shughuli ya 3.13
(a) Tazama igizo katika runinga au vifaa vingine vya TEHAMA, kisha hakiki
igizo hilo kwa kutumia nadharia ya uhalisia, huku ukiongozwa na maswali
yafuatayo:
(i) Ni kwa namna gani maudhui yaliyowasilishwa na wahusika katika
maigizo hayo yanaakisi hali halisi katika jamii?
(ii) Ni kwa namna gani uumbaji wa wahusika katika maigizo hayo unaakisi
hali halisi?
(iii) Maudhui yanayowasilishwa katika maigizo hayo yana athari gani kwa
jamii?
(iv) Je, lugha ya wahusika katika maigizo hayo ina uhalisi?
(v) Ni kwa namna gani mandhari ya maigizo hayo yanasawiri mazingira
halisi?
78 Kitabu cha Mwanafunzi
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 78 23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 78