Page 91 - Fasihi_Kisw_F5
P. 91
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
3. Macho yamtoka pima, John amekasirika,
Namuona anasema, “Baba ananitoroka?”
Ninabaki najiuma, nini kimempeleka,
FOR ONLINE READING ONLY
“Sikiliza John Chema”, ninamtoa mashaka,
“Nakwenda Moro tazama, wazazi wananitaka”,
John ananiambia, “hutan’acha Morogoro!”
4. Kwa dakika kumi nzima, John hasemi na mie,
Mgongoni aniuma, nusura nyama ang’oe,
Hapo nasogea nyuma, namvua an’achie,
Siwi tena na huruma, namshika nimtoe,
“Nakufa mwenzenu jama”, aita wamsa’die,
John ananiambia, “hutan’acha Morogoro!”
5. Nje ninapomtoa, namfungia mlango,
Hapo John analia, ajitupa kwenye dongo,
Gari anang’ang’ania, kama mchwa na udongo,
Mara anaiachia, imgusapo mgongo,
Huku anitamkia, atakamilisha lengo,
John ananiambia, “hutan’acha Morogoro!”
6. Sikose kuendelea, sehemu yake ya pili,
Ni nini kitatokea, Moro nitapowasili,
John ameshapania, kunif’ata kila hali,
Moro kanitamkia, atafika hatojali,
Tena kasisitizia, yeye mwanangu halali,
John ananiambia, “hutan’acha Morogoro!”
Diwani ya Mloka (Mloka, 2002: 28 - 29).
80 Kitabu cha Mwanafunzi
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 80
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 80 23/06/2024 17:54