Page 93 - Fasihi_Kisw_F5
P. 93
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
Mume
Mshahara unapewa, wako hauparuliwi,
Majukumu kugawana, napalangania denti,
FOR ONLINE READING ONLY
Bado pango nalipia, umeme na maji ni mimi,
Haya maisha ya ndoa, wenzangu mnaishije?
Mke
Mke si wa kuteseka, wangu sema asilani,
Zipunguze zako nongwa, kulalama hakufai,
Kucha nywele nasetia, kusaidia nyumbani,
Haya maisha ya ndoa, wenzangu mnaishije?
Mume
Mke msomi ni shida, wanaume tuna kazi,
Ya wahenga nikapuza, nikijua ni kejeli,
Viuno wajishikia, wanawaza ofisini,
Haya maisha ya ndoa, mwenzangu mnaishije?
Mke
Vyombo maji saidia, dawa tosha ya mapenzi,
Mke hawezi kutoka, atajituliza ndani,
Atakiandaa chanda, kando yatatengwa maji,
Haya maisha ya ndoa, wenzangu mnaishije?
Mwanamke ndege njiwa, apetiwe peti peti,
Asiguswe kwa mabaya, atapeperuka mbali,
Haloo wangu kibamba, toa maneno laini,
Haya maisha ya ndoa, wenzangu mnaishije?
82 Kitabu cha Mwanafunzi
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 82
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 82 23/06/2024 17:54