Page 98 - Fasihi_Kisw_F5
P. 98
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
George: Bado haujaelewa. Ninyi mko ndani ya madaraka yangu.
Martha: Nini?
George: Mko chini…
FOR ONLINE READING ONLY
Martha: Katika nyumba hii wewe huna madaraka yoyote! Tena
tafadhali ondoka.
George: Ond …
(Hakudhani kuwa Martha atasema hivyo)
Unajua unasema nini?
Martha: Nasema nini?
George: Labda huelewi. Herbert hakukueleza. Kimila, mimi ni mkubwa
wa Herbert. Mama yangu aliolewa, halafu mama aliyemzaa
Herbert.
Kwenye Ukingo wa Thim (Hussein, 2004: 24 - 28)
Maswali
(i) Mgogoro kati ya Martha na George unatokana na nini?
(ii) Kuna uhusiano gani kati ya mambo yanayosawiriwa katika kipande
hiki cha tamthiliya na jamii yako?
(iii) Kutokana na matini hii, ni kwa namna gani mwandishi anasawiri
matabaka na mifumo mbalimbali ya maisha katika jamii yako?
(iv) Jamii inapaswa kufanya nini ili kuepusha migogoro kama
inavyosawiriwa katika matini hii?
(v) Kwa namna gani matini hii imesawiri upiganiaji wa haki na suluhu
yake?
(vi) Utamaduni umeathirije maisha ya familia ya Herbert na Martha katika
matini hii?
(b) Hakiki tamthiliya moja teule kwa kutumia nadharia ya umaksi.
(c) Hakiki tamthiliya moja teule kwa kutumia nadharia ya mwingilianomatini.
Kitabu cha Mwanafunzi 87
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 87 23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 87