Page 102 - Fasihi_Kisw_F5
P. 102
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
Sura
ya Maadili katika fasihi
FOR ONLINE READING ONLY
Nne
Utangulizi
Maadili katika kazi za fasihi ni muhimu kwani husaidia kujenga mwenendo
na tabia inayokubalika katika jamii. Hivyo, kazi za fasihi zimekuwa chachu
ya kubadilisha jamii kupitia ujumbe unaopatikana katika kazi hizo. Katika
sura hii, utajifunza maadili yaliyomo katika nyimbo za bongo fleva, mashairi,
na tamthiliya. Pia, utajifunza misingi ya maadili, umuhimu wa maadili katika
jamii na maadili yaliyosawiriwa katika kazi za fasihi. Vilevile, utajifunza
namna ya kueleza na kuhusianisha mitazamo iliyomo katika kazi hizo za fasihi
na matendo ya jamii na athari za kiimani na kimtazamo zinavyodhihirika
katika jamii. Umahiri utakaoupata katika sura hii utakuwezesha kutunga
kazi za fasihi zenye kujenga maadili kulingana na mtazamo na imani ya jamii
husika.
Kazi za fasihi zinavyochochea ujenzi wa maadili katika
jamii
Maadili katika nyimbo za bongo fleva, mashairi na tamthiliya
Shughuli ya 4.1
Sikiliza au tazama nyimbo za bongo fleva kisha bainisha wimbo mmoja
unaodhani una maadili na wimbo mwingine unaodhani hauna maadili na eleza
kwa nini unasema wimbo fulani umezingatia maadili au la.
Maadili ni nini?
Maadili ni kanuni, miongozo na taratibu zilizowekwa na jamii ili kusimamia
mienendo na tabia za watu zinazokubalika katika jamii husika. Maadili huathiri
Kitabu cha Mwanafunzi 91
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 91 23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 91