Page 106 - Fasihi_Kisw_F5
P. 106
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
Hupendezwa kiongoke, cha kwake au cha kwetu,
Hupendezwa moyo wake, usitekwe mji wetu,
Japokuwa muudhike, yeye haogopi kitu,
FOR ONLINE READING ONLY
Shujaa haogopi kitu, kilicho halali yake.
Hodari nyumbani kwake, huwakaribisha watu,
Hutetea nchi yake, asiichafue mtu,
Yu tayari peke yake, kuutembelea mwitu,
Shujaa haogopi kitu, kilicho halali yake.
Mashairi ya Saadani (Kandoro, 1972:66)
Maswali
(i) Ni dhamira gani zinazopatikana katika shairi hili?
(ii) Kutokana na shairi ulilolisoma, unafikiri ni kwa namna gani maadili
yaliyomo yanaakisi jamii yako?
(iii) Ni kwa namna gani jina la shairi linaakisi maadili?
(iv) Unafikiri lugha iliyotumika inasawiri maadili ya jamii? Kwa nini?
(v) Mwandishi anamaanisha nini anaposema “Hodari kwa haki yake,
hapendi ipate kutu”?
(vi) Ni kwa namna gani mbinu za kisanaa zinaibua maadili katika shairi
hili?
(vii) Una mtazamo gani kuhusu maadili yanayoelezwa katika shairi hili?
(b) Chambua maadili yaliyomo katika mashairi mawili uliyosoma katika
diwani teule.
Maadili katika tamthiliya
Kutokana na kusoma au kutazama tamthiliya katika runinga, watu wamekuwa
wakijifunza mambo mengi yanayotokea au ambayo hayajapata kutokea katika
jamii zetu. Haya yote yanatoa mafundisho yenye kuadilisha kutoka katika
tamthiliya hizo na kuyaendeleza kwa manufaa ya jamii nzima.
Kitabu cha Mwanafunzi 95
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 95 23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 95