Page 105 - Fasihi_Kisw_F5
P. 105
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
Shughuli ya 4.2
(a) Kwa kutumia vyanzo vya mkondoni na vinginevyo, sikiliza wimbo wowote
wa bongo fleva unaosawiri umuhimu wa wazazi, au kusisitiza kazi au utu
wema kisha jibu maswali yafuatayo.
FOR ONLINE READING ONLY
(i) Ni dhamira zipi zinazopatikana katika wimbo huo?
(ii) Ni maadili gani yanayopatikana katika wimbo huo? (toa mifano)
(iii) Una mtazamo gani kuhusu wimbo huo?
(iv) Lugha iliyotumika katika wimbo huo inasawiri vipi suala la maadili?
(v) Wimbo huo una mchango gani katika kuhamasisha maadili ya jamii
ya Tanzania?
(b) Kwa kutumia vyanzo vya mtandaoni na vinginevyo, sikiliza nyimbo mbili
za bongo fleva, kisha chambua maadili yaliyomo katika nyimbo hizo.
Maadili katika mashairi
Waandishi wengi wamekuwa wakitunga mashairi yenye maudhui mbalimbali
yanayoshughulikia masuala ya kijamii. Mashairi yana mchango mkubwa katika
kutoa maadili mbalimbali yanayoelimisha na kuburudisha jamii.
Shughuli ya 4.3
(a) Chambua maadili yaliyomo katika shairi hili huku ukiongozwa na maswali
yanayofuata.
Shujaa haogopi kitu kilicho halali yake
Nisemayo muyashike, hili ni shairi letu,
Akuitae muitike, tuendeshe mambo yetu,
Shujaa na kitu chake, hadhulumiwi na mtu.
Shujaa hahofu kitu, kilicho halali yake.
Hodari kwa haki yake, hapendi ipate kutu,
Tena hageuki ike, japokuwa mwana kwetu,
Japo mtoto mshike, atafanya utukutu,
Shujaa haogopi kitu, kilicho halali yake.
94 Kitabu cha Mwanafunzi
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 94 23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 94