Page 110 - Fasihi_Kisw_F5
P. 110
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
Ulinganisho wa maadili na imani katika bongo fleva
Kwa upande wa fasihi, nyimbo nyingi za bongo fleva zimetumika kubeba maadili
yanayoendana na imani zilizopo katika jamii ya Watanzania ijapokuwa baadhi ya
nyimbo hizo zimekuwa zikikiuka maadili hayo na kasababisha kufungiwa.
FOR ONLINE READING ONLY
Shughuli ya 4.6
(a) Kwa kutumia vyanzo mbalimbali, sikiliza wimbo wa bongo fleva unaosawiri
umuhimu wa elimu, kisha jibu maswali yafuatayo:
(i) Ni dhamira zipi zinazopatikana katika wimbo huu?
(ii) Ni maadili gani unayoyapata kutokana na wimbo huu?
(iii) Ni imani zipi zinazodhihirika katika wimbo huu?
(iv) Kuna uhusiano gani kati ya maadili yaliyoelezwa na imani za jamii
yako?
(b) Tumia vyanzo vya mtandaoni au vinginevyo kusikiliza wimbo wa bongo
fleva, kisha linganisha maadili yaliyomo na imani za jamii.
Ulinganisho wa maadili na imani katika ushairi
Ushairi ni utanzu muhimu katika jamii kwani waandishi wengi wamekuwa
wakitunga mashairi yenye malengo ya kufunza, kuonya na kuadibu. Ushairi
hupata uhai wake kutokana na hali halisi za kijamii, ikiwa ni pamoja na imani
na maadili ya jamii husika. Hii inamaanisha kwamba utanzu huu hubeba maadili
yanayoendana na imani zilizomo katika jamii.
Shughuli ya 4.7
(a) Soma shairi lifuatalo, kisha linganisha maadili yaliyomo na imani za jamii
kwa kujibu maswali yanayofuata.
Mchwa na Kumbikumbi
Nchi yetu kichuguu, ndani yake tunaishi,
Tumbo letu na miguu, vyote ndani vinaishi,
Mawazo yetu kwa Mungu, aliyeweka utashi,
Kwa nini mwatunyanyasa, wakati wote twaishi?
Kitabu cha Mwanafunzi 99
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 99 23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 99