Page 115 - Fasihi_Kisw_F5
P. 115
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
Nimepewa na ardhi, natamka Tanzania,
Mola kwenu ameridhi, muweze kuitumia,
Wanafaidi baadhi, wengine wagugumia,
FOR ONLINE READING ONLY
Lakini Watanzania, wengi wenu ni wavivu.
Nimejaliwa asali, natamka Tanzania,
Afrika ni ya pili, kwa ubora mizania,
Hamfaidi kwa hili, nashangaa mnalia!
Lakini Watanzania, mnasikitisha mno.
Nimepewa na madini, natamka Tanzania,
Almasi na urani, dhahabu imetulia,
“Tanzanaiti” kundini, kwa faida yenu pia,
Lakini Watanzania, mmelala usingizi.
Nimejaliwa matunda, natamka Tanzania,
Mngeitafta tenda, kulisha Dunia,
Lakini mengi yavunda, huku mwayaangalia,
Lakini Watanzania kwa nini hamzinduki?
Nimejaliwa maji, natamka Tanzania,
Si ya kupikia uji, bali ya kumwagilia,
Maziwa, mito, “ulaji” kanitunuku Jalia,
Lakini Watanzania, bado mnalia njaa!
Nimepewa vivutio, natamka Tanzania,
Mbuga, Bahari patio, watu waifurahia,
Mngefanya kimbilio, leo mngeshangilia,
Lakini Watanzania, mwanikatisha tamaa.
104 Kitabu cha Mwanafunzi
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 104
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 104 23/06/2024 17:54