Page 116 - Fasihi_Kisw_F5
P. 116
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
Nimejaliwa misitu natamka Tanzania,
Mngepata vingi vitu, siyo kama natania,
Lakini hamthubutu, wanyonge nasimulia,
FOR ONLINE READING ONLY
Lakini Watanzania, mbona hamuendelei?
Kwa kweli nimemaizi, mama yenu Tanzania,
Pamoja na mali hizi, nyuma mnajirudia,
Wakiotesha mizizi, “weupe” mtajutia,
Lakini Watanzania, aliyewaroga nani?
Sibanduki (Hancha, 2015:16 - 17)
(b) Kwa kutumia mashairi mawili kutoka katika diwani teule, chambua
mitazamo inayopatikana katika mashairi hayo.
Mitazamo iliyomo katika tamthiliya
Katika kusawiri mambo halisi ya kijamii, tamthiliya, kama tanzu nyingine
za fasihi andishi, hudhihirisha mitazamo mbalimbali iliyomo katika jamii.
Mitazamo hiyo huwa na athari chanya au hasi katika jamii husika. Mitazamo
chanya ikisawiriwa vyema katika tamthiliya, hadhira hujifunza na kupata maarifa
mapya yanayowasaidia katika harakati zao za kuboresha maisha. Kinyume chake,
mitazamo hasi hurudisha nyuma maendeleo ya kijamii.
Shughuli ya 4.11
(a) Soma matini fupi ya tamthiliya ifuatayo, kisha jibu maswali yanayofuata.
Cheja: (kwa hamaki) Juma! Huwezi kwenda namna hii hata kidogo.
Huwezi kunikana na hali ulisema unanipenda. Nilikueleza
siku ile hatari yake hukutaka kunisikia. Ukajisingizia
mapenzi. Sasa leo unataka kunikana hivi. Hata kidogo!
Juma: Hata kikubwa. Usinishikilie hivyo. Tena nakueleza wazi
usije ukalogwa kumwambia mtu kuwa mzigo huo ni wangu.
Walahi utajuta.
Cheja: Utafanya nini?
Kitabu cha Mwanafunzi 105
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 105 23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 105