Page 118 - Fasihi_Kisw_F5
P. 118
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
Maswali
(i) Ni maudhui gani unayapata kupitia mazungumzo ya wahusika wa
matini hii?
(ii) Wahusika wana mitazamo gani katika matini hii?
FOR ONLINE READING ONLY
(iii) Unapata mtazamo gani kuhusiana na Cheja anaposema “Sembuli
alinikosea kwa nguvu na sasa mimi ni mjamzito”
(iv) Una maoni gani kuhusiana na matendo ya wahusika Cheja na Juma?
Je, yanapaswa kuigwa katika jamii? Kwa nini?
(v) Mitazamo gani inajengwa na matukio ya mhusika Juma?
(vi) Mbali na mitazamo iliyomo katika tamthiliya hii, una mitazamo gani
mingine kuhusiana na matini hii?
(vii) Unafikiri kuna uhusiano wowote kati ya mitazamo ya wahusika wa
tamthiliya hii na matendo ya jamii?
(b) Chambua mitazamo inayopatikana katika tamthiliya mbili teule ulizosoma.
Uhusiano wa mitazamo iliyomo katika bongo fleva, mashairi na
tamthiliya na matendo ya jamii
Kuna uhusiano mkubwa kati ya kazi za kifasihi na matendo ya jamii kwani
watunzi hutunga kutokana na matendo yanayofanywa na wanajamii. Uhusiano
wa mitazamo na imani ya jamii unaweza kuonekana katika baadhi ya kazi za
kifashi kama vile nyimbo za bongo fleva, mashairi na tamthiliya.
Uhusiano wa mitazamo iliyomo katika nyimbo za bongo fleva na matendo
ya jamii
Nyimbo za bongo fleva zimeonesha mitazamo mbalimbali inayosawiri matendo
ya jamii. Kwa kupitia usawiri wa matendo hayo wasanii wamekuwa wakitoa
mafunzo na maadili kwa jamii katika maeneo mbalimbali ya maisha. Wakati
matendo hasi yana athari mbaya kimaisha, matendo chanya yanaposawiriwa
vyema, wanajamii hupata maarifa yanayowasaidia kuleta mabadiliko chanya,
hivyo kuchangia kwenye ustawi na maendeleo ya jamii.
Shughuli ya 4.12
(a) Kwa kutumia vyanzo vya mkondoni au vinginevyo, sikiliza wimbo wowote
wa bongo fleva ulioimbwa na mtoto chini ya miaka kumi na minane (18),
kisha jibu maswali yafuatayo:
Kitabu cha Mwanafunzi 107
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 107 23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 107