Page 121 - Fasihi_Kisw_F5
P. 121
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
(b) Chambua mitazamo iliyomo kwenye mashairi mawili katika diwani teule,
kisha eleza namna inavyohusiana na matendo ya jamii.
Uhusiano wa mitazamo iliyomo katika tamthiliya na matendo ya jamii
Kama ilivyo kwa bongo fleva na mashairi, tamthiliya husawiri mitazamo na
FOR ONLINE READING ONLY
matendo ya wanajamii kama njia ya kujenga maudhui. Malengo ya maudhui hayo
ni kuleta mabadiliko katika jamii kwa kuonesha matendo na mitazamo chanya
kupitia wahusika wake. Hivyo, mazungumzo huwa ni malighafi ya msanii katika
kusana kazi yake.
Shughuli ya 4.14
(a) Soma matini fupi ya tamthiliya ifuatayo, kisha jibu maswali yanayofuata.
Bi Somoe: Mata mwanangu, sisi wazazi wako ni masikini. Lakini
hata siku moja hujasikia tumeiba mali ya ntu. Tusameheni
wanetu kwa kushindwa kuwasomesha. Ni sababu ya
umasikini wetu. Ingawa unajua kusoma mawili matatu.
Lakini huko njini uendako kama kuna uwezakano wa
kujiendeleza fanya hivyo. Kwani elimu haina mwisho.
Mata: Sawa mama.
Bi Somoe: Kila siku tunasikia kwenye maredio. Urithi wa ntoto ni
elimu. Zamani tuliona heri watoto wetu tuwatumikishe tu
kwenye mashamba ya mikorosho. Tulijua kuwa tungepata
faida kubwa. Kumbe ulikuwa ni ujinga. Ungekuwa na elimu
wala usingekwenda njini kwa mashaka. Ungekwenda njini
kwa kazi yako.
Che Munndu: Mama Mata unaongea nini? Wangapi wana elimu na
wanaishi kwa mashaka?
Bi Somoe: Kwani kuoa ni ujanja? Au kuoa wake wengi kila kukicha
na kuwa na watoto wengi kama bata ndo ujanja?
Che Munndu: Sasa hiyo unaona ni ujinga? Ndo maana kila mwananke
ninayemwoa nampa talaka sababu ya ulozi wako.
Bi Somoe: Nlozi we mwenyewe. Unaoa kila ukipata hela za
korosho. Wanawake wanajua una pesa. Pesa zikikuishia
wanakukimbia. Mbona mi uliyenioa na umaskini
sikukimbii?
110 Kitabu cha Mwanafunzi
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 110
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 110 23/06/2024 17:54