Page 117 - Fasihi_Kisw_F5
P. 117
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
Juma: (Anacheka). Eti “utanifanya nini” kwanza utaniona wapi?
Kwanza nani shahidi?
Cheja: (kwa uchungu). Yaani kweli, Juma imekuwa si kitu kwako
litakalonipata baadaye. Hunifikirii nitamfanyaje mtoto.
FOR ONLINE READING ONLY
(Anashindwa kusema kwa muda.) Kumbe yote yalikuwa
ulaghai mtupu. Siamini! Siamini!
Juma: Amini! Amini tu! Wewe sikiliza. Jiendee zako kwa wazazi
wako ukajitunze kama unaogopa kuendelea kukaa kwa
mwajiri wako. Nenda tu.
Cheja: Sikuweza kuvumilia kukaa tena nyumbani kwao.
(Anatazama chini.) Hapana sikuweza.
Bw. Chowe: Kwa nini?
Cheja: (Kwa kusita hali akiwa bado anatazama chini.) Bwana Se
… Bwana Sembuli alinikosea kwa nguvu na sasa mimi ni
mjamzito…
Cheja: Bwana Sembuli alinikosea kwa nguvu na sasa mimi ni
mjamzito. (Wote wanapigwa bumbuazi).
Bw. Chowe: Eti nini? (Cheja anaanza kulia).
Bi. Chowe: Uuuuuui, Uuuuuuuuuui Mungu wangu! (kwa wanawake
wenzie) Jamani nielezeni labda sikusikia vizuri.
Uuuuuuuuuuuuui! (Anamkimbilia Cheja). Cheja mwanangu
Uuuuuuuuuuui!
Bw. Chowe: (kwa Bi. Chowe) Aaa! Acha kelele wewe. Sema vizuri
Cheja sema acha kulia! Ati kweli au unatania?
Cheja: Kweli baba.
Bi. Chowe: Uuuuuuuuui! Uuuuuuuuuui! (Anakwenda kwa wanawake
wenziwe). Uuuuuuui!
Hatia (Muhando, 1974: 9-15).
106 Kitabu cha Mwanafunzi
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 106
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 106 23/06/2024 17:54